MWANAMITINDO maarufu Bongo, Martin Kadinda amesema
kabla hajawa kiongozi wake, awali aliwahi kumtamani kimapenzi mcheza
filamu Wema Sepetu, lakini alighairi baada ya kugundua ni mwanamke wa
kudekadeka.
Kadinda alitoa kauli hiyo hivi karibuni wakati akipiga stori na
paparazzi wetu kuhusu masuala mbalimbali yanayomhusu msichana huyo
ambaye ana uhusiano wa kimapenzi na mkali wa Bongo Fleva, Diamond
Platinumz.
Kuhusu maisha wanayoishi nyota hao wawili wapenzi, Kadinda alisema
kwa jinsi wanavyoishi ni kama watu wanaoigiza, akitolea mfano wa kipindi
walichorudiana wakiwa nchini China, ambako wenyewe walisema wanaigiza
filamu wakati ndiyo kwanza walikuwa wanarejesha penzi lao lililovunjika
mara ya kwanza.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment