MWANAMUZIKI aliyefariki dunia, Amina Ngaluma maarufu
kama Japanese alifikisha siku 40 tokea azikwe Jumamosi iliyopita,
lakini katika kisomo kilichosomwa nyumbani kwao Kitunda, hakuna staa
yoyote wa muziki wa dansi aliyehudhuria.
Japanese alifariki dunia mwezi uliopita nchini Thailand alikokuwa
akifanya kazi ya muziki na katika shughuli hiyo ya wiki iliyopita,
masheikh mbalimbali walihudhuria kwa kisomo kabla ya kufuturisha watu.
Kabla ya mauti kumfika, Japanese aliwahi kufanya kazi kwa kujituma
katika bendi za African Revolution ‘Tam Tam’, Double M Sound na TOT,
lakini katika hali ya kusikitisha hakuna hata mwanamuziki mmoja
aliyehudhuria zaidi ya mumewe, Rashid Sumuni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment