KICHEKESHO: MASWALI YA KIJINGA NA MAJIBU YA KIPUZI!!!


1.SWALI: Ni mvua inanyesha?
JIBU: Hapana ni supu yamwagika.

2. SWALI: Hilo ni gazeti la leo?
JIBU: Hapana ni langu.

3.Mwalimu mkuu:Umemwona headboy?
MWANAFUNZI: Sikuwa namtafuta.
... 
4.SWALI: Unakula?
JIBU: Hapana nabusu kijiko!

5. SWALI: Unangoja lift uende juu?
JIBU: Hapana nangojea ofisi ishuke chini!

6. SWALI: We ndo wa mwisho mstarini?
JIBU:Hapana mi ndio wa kwanza tumesimama kinyumenyume!

7.SWALI: Umeamkaje?
JIBU: Kwa kufungua macho na kushuka kitandani kwa miguu yangu mwilini!

8.SWALI(mama anauliza mtoto wake):Unataka kulia nn?
Jirani Kamjibu:Labda amechoka na kushoto!

9.SWALI: Unalala?
JIBU: Hapana napractise kufa!

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger