Katika hali yakushangaza, Lucas Mkenda au maarufu kama Mr.Nice, finaly
afunguka kuhusu utajiri wake na sababu za kushuka kwake kimuziki, katika
moja ya interview Mr.Nice alidai kuwa hajui ni nini haswa kilichotokea
ila yote hayo ni mipango tu ya Mungu.Mr.nice alizidi kufunguka na kusema
kuwa, alikuwa na jumla ya zaidi ya shilingi bilioni 1.5 zote zikiwa
katika account mbalimbali hapa nchini, na hela zote hizo zimetoweka
katika kipindi cha muda mfupi bila yeye kujua zimetumikaje.
“kaka naweza kusema hii ni mipango ya Mungu tu, kwani sikuwahi
kumdhulumu mtu wala kuiba cha mtu, pesa yote nilikuwa naipata kwa hali,
naweza kusema hii ni mipango ya Mungu tu wala si mkono wa mtu” alisema
Mr.Nice.
“Niliwahi kumiliki zaidi ya milioni elfu moja na mia tano kwenye bank
tofauti hapa nchini, pesa hizo zilitokana na kufanya shoo nyingi za nje
ya nchi kama. Marekani,Uingereza, Ujerumani, Sweden, Holand, Dubai,
SouthAfrica na kwingineko, na kila shoo nilikuwa napata pesa ndefu sana”
Alimalizia star huyo kutoka Tzee na mwanzilishi wa staili ya TAKEU.
`
Mbali na kushuka kwake kimuziki Mr.Nice anakiri kuwa ana-miss sana enzi
hizo kwenye show zake zisizoweza kusahaulika na machozi huwa yanamtoka
kila akumbukapo show aliyopiga nchini Rwanda ambapo hadi waziri wa
nchini humo aliweza kumsubiria airport kumpokea tena kwenye red carpet
huku akisindikizwa na magari ya polisi, pamoja na mashabiki wake lukuki
waliojaza uwanja huo wa ndege kushuhudia ujio wake.
No comments:
Post a Comment