MAI AVISHWA PETE YA UCHUMBA, NDOA KUFUNGWA UPYA

MTANGAZAJI ambaye kwa sasa anafanya dili za ujasiriamali, Maimartha Jese ‘Mai’hivi karibuni alivishwa upya pete ya uchumba na ya ndoa baada ya zile za wali kupotea katika mazingira ya kutatanisha.
Mtangazaji ambaye kwa sasa anafanya dili za ujasiriamali, Maimartha Jese ‘Mai’
Aliyemfanyia tukio hilo ni mumewe aitwaye Shaa na baada ya vidole vyake kupendeza tena alitupia picha akiwarusha roho mashoga zake na alipoulizwa na paparazzi wetu juu ya pete hizo alisema, mume
wake ndiye aliyeamua kumvisha baada yakuona ni heshima kwa mke wa mtu.

“Nimejisikia furaha sana kwani ilikuwa ikininyima raha kuona pete za mume wangu hazipo tena kidoleni, sasa nina amani tele,” alisema Mai

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger