UZEMBE! Josephine Josin (19), mkazi wa
Morogoro ambaye anafanya kazi ya uhudumu wa baa iliyopo maeneo ya Mji
Mpya, mkaoni hapa, amedaiwa kumgonga na gari muuza mahidi aliyefahamika
kwa jina la Pori wakati akifundishwa gari na mpenzi wake.
Kwa mujibu wa mashuhuda, tukio hilo lilitokea hivi karibuni ambapo
dereva wa gari aina ya Toyota Noah lenye namba T 63* CVE, Alfa Ibrahimu
alikuwa akimfundisha Josephine ndipo alipomgonga Pori.“Awali tulimshuhudia huyu baamedi akinywa pombe na huyu dereva wa Noah, baada ya kufunga baa majira ya saa 3 usiku, akaingia kwenye Noah akaendesha huku akiwa amelewa na dereva aliyekuwa akimfundisha (Alfa) naye alikuwa amelewa.
“Tuliwatazama tu lakini ghafla alikanyaga
mafuta kwa nguvu na gari ikaruka na kumvaa mzee anayeuza mahindi (Pori)
na kutokea upande wa pili ikagonga bucha langu,” alisema Mazengo.
Akizungumza na mwandishi wetu mara baada ya kutoka hospitali
alipolazwa kwa muda, mzee Pori alisema alipata majeraha madogo katika
paji la uso na wahusika walimfuata na kumlipa Sh 40,000 kama gharama za
matibabu pamoja na mtaji wake wa mahindi.Akihojiwa na mwandishi wetu kuhusiana na tukio hilo, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mkoa wa Morogoro, Boniface Mbao alikiri kutokea kwa tukio hilo ila akasema yeye si msemaji, aulizwe Kamanda wa Polisi wa Mkoa ambaye hakuweza kupatikana mara moja.
No comments:
Post a Comment