MASIKITIKO: KIJANA MWINGINE AFA JKT




Nimepokea kwa masikitiko makubwa msiba wa Raphael Kingaz aliyekuwa mwanafunzi wa HGE shule ya sekondari mbezi beach, mauti yamemkuta akiwa Tanga kwenye kambi ya mafunzo ya JKT.

Mtoa taarifa wangu wa kuaminika aliyezungumza mtandao huu jamvilahari.com alisema mauti yalimfika jana jioni na mazishi yanatarajia kufanyika kesho. sababu ya kifo chake bado hatujaipata.



Pole ziwafikie ndugu, jamaa na marafiki na jumuiya yote ya shule ya sekondari mbezi beach



HAPA CHINI NI TAARIFA ILIYOTOLEWA NA JKT KUKANUSHA VIFO VINAVYOTOKEA JKT HAVITOKANI NA UKATILI

TANGAZO
JESHI LA KUJENGA TAIFA, LINAKANUSHA TAARIFA ZINAZOSAMBAZWA KWA KUTUMIA UJUMBE MFUPI WA MANENO (SMS) KATIKA SIMU ZA VIGANJANI NA MTANDAO WA JAMIIFORUM.COM, KWAMBA VIJANA WA KUJITOLEA NA MUJIBU WA SHERIA WANAOENDELEA NA MAFUNZO KATIKA MAKAMBI YA JKT WANAKUFA KWA UKATILI, WAKITOLEA MFANO KAMBI YA JKT OLJORO ARUSHA KWAMBA KUNA VIJANA WATATU WAMEFARIKI DUNIA.

UMMA UFAHAMU KUWA TAARIFA HIZO SI ZA KWELI NI UPOTOSHAJI KWA VIJANA NA WATANZANIA. UKWELI NI KWAMBA KUNA KIJANA MMOJA WA KIKE HONORATA VALLENTINE OISO ALIYEFARIKI KATIKA KIKOSI CHA JKT OLJORO ARUSHA KWA UGONJWA WA UPUNGUFU WA DAMU (ANAEMIAULIOSABABISHWA NA MALARIA. SIO VIJANA WATATU KAMA INAVYOELEZWA KWENYE UJUMBE UNAOSAMBAZWA. WAZAZI WA KIJANA ALIYEFARIKI PIA WALITHIBITISHA KUWA KIJANA WAO ALIKUWA NA MATATIZO YA UPUNGUFU WA DAMU.

JESHI LA KUJENGA TAIFA LINASISITIZA KUWA HAKUNA UKATILI WOWOTE UNAOFANYWA KWA VIJANA WANAOENDELEA NA MAFUNZO KATIKA MAKAMBI YA JKT.

JKT LINALAANI KITENDO HICHO NA LINAFUATILIA ILI KUBAINI CHANZO CHAKE. MTU YEYOTE ATAKAYEBAINIKA KUWA NDIYE CHANZO CHA UJUMBE HUO, HATUA ZA KISHERIA ZITACHUKULIWA DHIDI YAKE.

JESHI LA KUJENGA TAIFA LINAWAKUMBUSHA VIJANA NA WATANZANIA KUWA MAKINI NA MATUMIZI MABAYA YA SIMU ZA MIKONONI NA MITANDAO YA JAMII, HASA KWA TAARIFA ZINAZOHUSISHA JESHI.

TANGAZO HILI LIMETOLEWA NA MAKAO MAKUU YA JKT

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger