MASKINI Mungu wangu! Ndiyo maneno aliyoanza nayo
kusema mama mzazi wa mtoto Salome Abdallah Said (3), kutokana na mwanaye
huyo afya yake kuzidi kubadilika kufuatia kuumwa mara kwa mara licha ya
kufanyiwa upasuaji mara mbili.
Akizungumza na gazeti hili wiki iliyopita mama wa mtoto huyo Veronica
Laurent, mkazi wa Bunju B, jijini Dar es Salaam alisema kwamba mwanaye
kwa sasa hali yake siyo nzuri kwa vile amekuwa akijisaidia haja kubwa
kupitia mdomoni kama hapo awali, hali hiyo anasema ameambiwa na
madaktari inasababishwa na utumbo wake wa haja kubwa kujikunja.
HISTORIA YA MTOTO
Veronica anaeleza: “Mwanangu kwa sasa ana miaka
mitatu, tangu nimzae katika Hospitali ya Mwananyamala, Dar,
aligundulika ana matatizo ya kutojisaidia haja kubwa kama kawaida
ilibidi nipelekwe Hospitali ya Muhimbili kwa uchunguzi zaidi.
“Nilimfikisha Muhimbili akiwa katika hali mbaya akawa anajisaidia
haja kubwa kupitia mdomoni, hata hivyo, nikaambiwa tumpeleke Hospitali
ya Agha Khan kwa vipimo zaidi, huko akagundulika kuwa utumbo wa haja
kubwa umejikunja.”
AFANYIWA UPASUAJI MUHIMBILI
Katika maelezo yake mama huyo alisema
kwamba mtoto wake alifanyiwa upasuaji kwa mara ya kwanza tumboni na
kuwekwa tundu ambalo alikuwa akilitumia kutolea haja kubwa, baadaye
akafanyiwa tena upasuaji kwa mara ya pili chini ya tumbo na kuwekewa
utumbo bandia lakini hata hivyo, ulikuwa mwembamba hivyo ukawa haufanyi
kazi vizuri.
UTUMBO WA BANDIA
“Tulipotoka Muhimbili na kurejea nyumbani
haikuchukua siku nyingi hali ya mtoto ikazidi kuwa mbaya, akawa analia
kila mara nikaamua kurudi Muhimbili.
“Madaktari baada ya uchunguzi wakasema utumbo wa bandia aliowekewa
ulikuwa mdogo na mwembamba hivyo ulishindwa kufanya kazi pia utumbo
ulikuwa umejikunja.
“Niliambiwa zinahitajika shilingi laki tisa ili
afanyiwe matibabu ambapo nimeshindwa kuzipata, bora awamu ya kwanza
alijitokeza mdhamini akatoa shilingi laki tisa. Nawaaomba Watanzania
wenzangu wamsaidie mwanangu ili kumnusuru na kifo, maana madaktari
wamesema bila kufanyiwa hivyo anaweza kupoteza maisha,” alisema mama
huyo.
Akifafanua zaidi alisema: “Wakati fulani ili apitishe haja kubwa
katika njia ya kawaida inabidi ninunue dawa ya kulainisha kinyesi kwani
bila kufanya hivyo ni lazima ajisaidie kwa kupitia mdomoni.”
BABA YAKE ATOROKA
“Kwa sasa mtoto halali kutokana na kulia
kutokana na maumivu makali, baba yake baada ya kuona tatizo la huyu
mwanangu alitoweka na kuzima simu, hapatikani. Mimi nashindwa kufanya
kazi yoyote.
Nawaomba Watanzania mnisaidie kupitia namba yangu ya
simu 0712 004 677 au 0767 026 551,” alisema mama huyo huku
akilengwalengwa na machozi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment