Akiwa anahojiwa na jarida moja la huko nchini Kenya Vanessa Mdee,
afunguka mengi ambayo hajawahi kuyasema sehemu nyingine yeyote ile, na
kwa wengi wanaomfahamu mkali huyu wa anayezidi ku-make headlines na
single yake ya “hawajui”, watabaki midomo wazi kwa vile ambavyo walikuwa
hawavijui kabisa kuhusu mwanamuziki huyu kutoka Tzee.
-Moja ya mambo ambayo vanessa huwa hafanyi kabisa mbali na kuwa
mwanamuziki, mtangazaji na mwanaharakati ni kupika, Vanessa alifunguka
na kusema hata akiwa nyumbani kwake ishu nzima ya kupika haimjii akili
kabisa. Tofauti na wanawake wengi wa afrika, hii ishu ni moja kati ya
vitu vilivyotokea kuwashangaza wapenzi wengi na wadau wanao mzimia
Vanessa.
-Siku alipotoa hit single yake ya “hawajui”, Hii ni moja ya single
aliyoitoa kwa watu ambao walikuwa hawamkubali hasa baada ya maneno yao
kuzidi kusema kuwa Vanessa hakustahili tuzo ya Kilimanjaro Music Awards
aliyoipokea na wengine kusema hakuwa teyari kupokea tuzo hiyo, jambo
hili lilimhuzunisha sana Vanessa, hii ilimsukuma vanessa kuandika kuhusu
watu wale ambao walikuwa hawamkubali(Haters), na kutoa kitu hiki
kinachozidi ku-make headlines kila siku.
-Moja ya mabo ambayo yaliwahi kumshangaza yeye mwenyewe vanessa kama
mtangazaji, ni siku alipokuwa ameenda kufanya mahojiano na kiongozi
Olesegun Obasanjo, alifunguka na kusema kwamba alipokuwa anamuhoji
wajukuu wake walikuwa wakicheza, huku wakimpiga makofi babu yao, Vanessa
ilimbidi kushangaa kile alichokuwa anashuhudia, hasa ni jinsi gani
kiongozi huyu mkubwa kama yeye anayeheshimika kuzidi kupigwa na wajukuu
zake, huku akicheza nao.
-Vanessa alifunguka na kusema kuwa umaarufu kama wake unakuja na faida
zake mbali na kuwa na vikwazo vingi katika kazi, moja ya faida zake ni
kuwa huwa mara nyingi hapangi foleni anapoenda mahali, alizidi kufumguka
na kusema siku moja aliwahi kushikwa na polisi barabarani kwa kutofunga
mkanda akiwa anaendesha, polisi alivyofika pale Vanessa aka-smile tu na
kumuomba msamaha na officer yale akabidi amuachie tu.
-mbali na kufunguka kote huko Vanessa anasisitiza kuwa ni vizuri kwa mtu
kutokata tamaa katika ndoto zako, kama alivyosema Lupita, siku moja
matunda ya ndoto zako zinaweza kuwa kweli. Vanessa ni mmoja ya watu
maarufu wacache wenye vipaji vingi, mbali na muziki hujihusisha na
utangazaji wa redio, MC katika sherehe mbalimbali kubwa,ukiacha mbali
uanamuziki na harakati zake katika jamii zinazohusu kuelimisha jamii juu
ya ukimwi na jinsia.
No comments:
Post a Comment