Ingawa siku zote za maisha yetu hapa
duniani tunatakiwa kuacha kutenda dhambi, kufanya mambo ya kumpendeza
Mungu na kuwa watu wema, lakini mwezi huu umefanywa kuwa maalum zaidi na
uzoefu wa kimazingira unaonyesha kuwa matendo maovu kama wizi, ubakaji,
biashara ya uchangudoa na uhalifu mwingine hupungua kwa kiwango
kikubwa.
Kupungua kwa matukio ya kihalifu na
ukosefu wa maadili wakati wa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani
unathibitisha kitu kimoja kuwa, kama binadamu, tunao uwezo wa kujizuia
kufanya matendo maovu, lakini huenda ni kwa vile tunao udhaifu mkubwa wa
kibinadamu, unaotufanya tujikute tukipotoka.
Ingawa ujumbe huu ni kwa watu wote,
ndugu zangu Waislamu na wasio Waislamu, lakini ni maalum zaidi kwa
mastaa wetu wa fani mbalimbali, kuanzia wanamichezo na wasanii, kwa
sababu wao ndiyo wanaoiwakilisha jamii inayowazunguka.
Kuna msemo unaosema msanii ni kioo cha
jamii. Sina uhakika kama wasanii wenyewe wanajua nini maana ya msemo
huu. Kwa kuwasaidia, huu ni msemo wenye maana kubwa sana kwao kwani wote
tunajua kioo kilivyo, ukijiangalia unajiona.
Huwezi kujitazama halafu ukajiona tofauti na ulivyo.
Tunaposema wao ni kioo cha jamii, tunamaanisha tukiwatazama, jinsi wanavyoishi, wanavyozungumza, wanavyovaa na kila wanachokifanya, basi hivyo ndivyo jamii yao ilivyo.
Tunaposema wao ni kioo cha jamii, tunamaanisha tukiwatazama, jinsi wanavyoishi, wanavyozungumza, wanavyovaa na kila wanachokifanya, basi hivyo ndivyo jamii yao ilivyo.
Lakini matendo ya baadhi ya wasanii
wetu, jinsi wanavyovaa mavazi yao ya nusu utupu, wale akina kaka
wanaovaa chini ya makalio, akina dada wanaosagana, wanaume wanaoshiriki
mapenzi ya jinsia moja, wanaotumia madawa ya kulevya na mambo mengine
yasiyo na maadili, hayawakilishi taswira halisi ya Mtanzania
tunayemfahamu.
Itashangaza, kwa mfano, kusikia msanii
mmoja mwenye mwili mkakamavu, amempiga binti mrembo mangumi baada ya
kuwa amezidisha dozi ya sigara zao za kikubwa na wala hatutegemei
kusikia eti watu wamekutana klabu na kuamua kupigana baada ya kulewa.
Ni wakati wa kujiangalia upya na kuchuja
baadhi ya matendo ambayo hayampendezi Mungu, ili aweze kuwapa rehema,
afya, nguvu na hata akili ya kuweza kuyapeleka maisha yao katika njia
inayostahili. Wasanii wetu wengi, pamoja na fursa nyingi wanazokutana
nazo katika harakati za kazi zao, bado wamekuwa hawana mipango madhubuti
ya namna ya kujiweka vizuri kwa ajili ya kesho.
Kama ni lazima twende klabu usiku na
kwamba hatuwezi kulala bila kupasha, basi siyo jambo baya kupunguza
kiasi cha kiburudisho unachotumia, ili kutoa nafasi kubwa ya kutojikuta
ukigeuka habari. Huu uwe ni mwezi ambao unaweza kubadili kabisa maisha
yetu.
Binadamu huishi kwa kujifunza na huwezi
kubadili maisha yako kama huwezi kubadili baadhi ya tabia. Wengi
wanafanya mambo kwa sababu ya kutaka sifa, kuogopa kuonekana wamefulia
au kuiga. Huu ni ujinga.
Kama umetumia mamilioni ya fedha kwa
ajili ya kwenda kula maisha katika klabu za usiku kwa miaka mingi,
hujachelewa kama sasa utasitisha safari hizo mwezi huu ili ujikague uone
kama utakuwa umefanya jambo la maana au la!
No comments:
Post a Comment