Kama kawaida, wiki iliyopita tulimleta kwenu staa wa Bongo
Fleva, Meninah Abdukareem ‘Ladiva’ ambapo mlituma maswali yenu na leo
haya ndiyo majibu yake, UNGANA NAYE...
RUSHWA YA NGONO BSS
Meninah kwanza nakupa big up kwa utulivu
ulionao mpaka sasa, je, kwenye mchujo wa kupata mshindi wa BSS (Bongo
Star Search), eti kuna rushwa ya ngono na fedha? John Ipembe, Shinyanga,
0713554815
MENINAH: Asante, BSS hakuna kitu kama hicho.
ANAOMBA NAFASI
Meninah nimekufuatilia muda mrefu, nimeona ni msichana mtulivu, naomba nafasi niwe mtu wako. Muddy Madiley, 0652672805
MENINAH: Bado muda sijaamua kuwa kwenye uhusiano ila nashukuru kwa kunifuatilia.
MPANGO WA KUOLEWA
Pongezi nyingi kwako dada Meninah kwa kufanya
vizuri katika gemu ila napenda kujua una mpango wa kuolewa? Amiri
Salumu, Dar, 0653252416
MENINAH: Asante kwa pongezi, mpango wa kuolewa kwa sasa bado kama nitakuwa nao nitawaambia.
HUYU ANATAKA KUJUA
Eti Meninah wewe ni mwenyeji wa mkoa gani na mbali na muziki unajishughulisha na nini? Salim Liundi, Dar, 0659601205
MENINAH: Mimi ni mwenyeji wa Dar, tofauti na muziki nafanya shughuli za
kibiashara, nafanya kazi kwenye media house (chumba cha habari) moja
hivi pia ninasoma.
MAFANIKIO
Eti dada umepata mafanikio gani kwenye muziki? Mama Daud, 0716692880
MENINAH: Nimepata fursa nyingi na kuonana na watu muhimu, nimevuka boda
pia nimenunua gari kwa kupitia fedha nilizopata kwenye muziki.
HUYU ANAHOJI
Meninah ni kweli mama yako ni Mhaya na anaitwa Eva
na kama ndivyo hilo jina la Abdukareem limetoka wapi? Noel Mushi, Moshi,
0714300280
MENINAH: Mama yangu siyo Mhaya ni Mhehe, jina la Abdukareem ni la baba yangu.
ANAOMBA NAMBA YA SIMU
Dada naomba namba yako ya simu tuwe tunawasiliana, nimekupenda sana. Sayuma Yusuf, 0657052463
MENINAH: Hapana, kutoa namba ni vigumu naomba uwasiliane nami kupitia Mtandao wa Instagram natumia jina hili Meninaladiva.
ETI ANACHEPUKA NA MSHINDI WA BSS 2013?
Dada kuna taarifa zilienea
mtaani kuwa wewe una uhusiano wa mchepuko na mshindi wa BSS 2013, je,
ni kweli? Said, Dar, 0718000790
MENINAH: Hakuna kitu kama hicho.
AMEHAMIA SKYLIGHT BAND?
Nakukubali sana dada Meninah, hivi umehamia Skylight Band? Rabia Mohamed, Dar, 0659985793
MENINAH: Hapana sipo ila kuna rafiki yangu ambaye tunafanana sana
anaitwa Digna ndiye yupo Skylight na watu wengi wanatuchanganya.
ANAMFAHAMU
Nakufahamu Meninah umezaliwa Manzese Uzuri (Dar), mama yako anaitwa Amina Mkwawa, baba yako Abdul Atik. Msomaji, 0715059450
MENINAH: Siyo kweli.
ANAMHOJI
Napenda sana kazi zako, je, una mchumba na vipi kuhusu ndoa? Msomaji, 0716784168
MENINAH: Sina mchumba na bado sijaamua kuolewa.
YEYE NA OMMY DIMPOZ
Meninah eti ni kweli unatoka kimapenzi na Ommy Dimpoz? Francisca, Tanga, 0652332243
MENINAH: Hapana.
ETI ANA MASHAUZI
Hooo! Dada nakujua tulikuwa wote kwenye BSS 2013
ulikuwa na mashauzi hata hutaki kuongea na watu pwaaa. Jenipher
Charles, Dar, 0755075255
MENINAH: Sikufahamu na sijawahi kushiriki na mtu mwenye jina hili, sina mashauzi.
AMEFAIDI NINI BSS?
Vipi Meninah umefaidika nini ulivyoshiriki BSS
na ulifika steji ipi na una mpango gani na maisha ya baadaye? Erasto,
Moshi, 0752387512
MENINA: BSS imenisaidia kujulikana na vyombo vya
habari, kama siyo ningepata ugumu sana wa kazi zangu kujulikana, kuhusu
mpango wa maisha yangu ni kuwa na familia yangu niwe na kwangu kwani
sasa hivi nipo nyumbani kwetu.
HUYU ANAMFAHAMU
Meninah ulikuwa unakaa Kurasini karibu na Uhamiaji, ulikuwa unatoka na madereva teksi kabla hujawa maarufu. Msomaji, 0713388514
MENINAH: Ni kweli tumeishi huko Kurasini lakini kuhusu kutoka na
madereva teksi siyo kweli kwani mama yangu alikuwa na gari hivyo wakati
akiwa hayupo tulikuwa tukiendeshwa na dereva teksi mmoja hivi ambaye
mama alikuwa akimuomba atupeleke mjini.
USHAURI
Dada ninakushauri kwamba wewe ni binti mzuri sana
jiepushe na skendo kama hawa wasanii wengine leo wana hili kesho lile,
jiheshimu kama mtoto wa kike nawe utaheshimika, uzuri wako uendane na
tabia yako.
Rejina Musa, Arusha, 0767909535
MENINAH: Asante kwa ushauri nitaufanyia kazi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment