MAKUBWA! Staa wa filamu na muziki Bongo, Baby Madaha
anadaiwa kwenda kijijini kwao kutambika baada ya kuona mambo yake
yanamwendea kombo.
Akizungumza na mwanahabari wetu, rafiki wa karibu wa Baby Madaha
ambaye hakupenda kuanikwa, alisema kutokana na staa huyo kuona mambo
hayaendi vizuri hasa kwenye muziki, ameamua kwenda nyumbani kwao Mwanza
kwa ajili ya kutambikia mizimu ya kwao.
Alipotafutwa Baby kuhusiana na ishu hiyo, alifunguka:
“Ni kweli
niko nyumbani kwetu Mwanza, ni muda mrefu sijaja kumuona mama, kuhusu
kutambika hilo ni lazima kwani nikiona mambo hayaendi vizuri, lazima
niikumbuke mizimu ya kwetu,” alisema Baby.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment