MWIGIZAJI wa filamu Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’
amesema amewaunga mkono Waislamu kwa kuvaa mavazi ya kujistiri na
kuziba sehemu kubwa ya mwili kuheshimu mwezi wa Ramadhani.
Akipiga stori mbili tatu na paparazi wetu, Johari alisema ameamua
kufanya hivyo kwa sababu dini zote ni za Mungu na kwa kuwa ni kipindi
cha Ramadhani, amebadilika kwa kila kitu.
“Kipindi hiki ni cha kumrudia Mungu, nimeacha kila kitu kibaya kwa
kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani na nimeamua kutulia ili
nipate muda mwingi wa kuomba,” alisema Johari.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment