Stori: Erick Evarist
WAKATI Arobaini ikitarajia kufanyika jana, mchumba
wa marehemu Sheila Haule ‘Recho’, George Saguda ameeleza kuwa bado
aliyekuwa mchumba wake huyo anamtesa kwa kumtokea mara kwa mara.
Akizungumza na mwanahabari wetu, Saguda alisema marehemu amekuwa
akimtokea akiwa usingizini na kumsisitiza kuhusu kazi.“Najitahidi sana
kuondoa mawazo juu yake lakini bado ananitokea, sijui hali hii itaisha
lini,” alisema Saguda.
Recho kabla hajapatwa na umauti, walizalisha filamu mbili katika
kampuni yao ya Sara Entertainment ambazo ni Vanessa na Fedheha ambayo
imetoka hivi karibuni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment