Tume
inayodhibiti taarifa za umma nchini Uingereza inafanya uchunguzi iwapo
mtandao wa Facebook ulivunja kanuni zinazolinda data ya watu binafsi.
Hii ni baada ya taarifa kuibuka kuwa Facebook iliwafanyia watu utafiti wa kisaikolojia bila idhini yao.
Afisi
ya mkuu wa habari wa tume hiyo alisema kuwa kuwa shirika hilo lilikuwa
limepanga kuihoji Facebook kuhusu utafiti huo.Katika utafiti huo,
Facebook ilichunguza taarifa za watu wapatao 700,000 ili kudhibiti hisia
ilizotaka kutoka kwao.
"Tunafurahia kujibu swali lolote walilo nalo wadhibiti," Richard Allen wa Facebook alisema katika ripoti moja.
Majarida
ya 'The Financial Times' pamoja na 'The Register' yalinakili kuwa afisi
hiyo ilisema kuwa ingewasiliana na shirika la kudhibiti data la Irelend
kuhusiana na swala hilo.
Facebook ina moja ya makao yake jijini Dublin.
'Utafiti wa Hisia'
Utafiti
huo uliendeshwa pamoja na chuo kikuu cha Cornell na vile vile chuo
kikuu cha Carlifornia jijini Sao Paulo kwa watumizi 689,000 wa Facebook
kwa muda wa juma moja mwaka wa 2012.
Kwa mujibu wa ripoti ya utafiti huo: "uchunguzi huo uliendeshwa kwa kiwango ambacho taarifa za faragha za watu zilifichuliwa.''
Utafiti
huo ulionyesha kuwa watumizi waliokuwa na taarifa chache hasi katika
mtandao wao hawakuandika kwa urahisi taarifa mbaya, na kinyume chake.
Kadhalika
utafiti huo ulifanywa ili kupima iwapo "tabia ya mtu kuandika katika
ukurasa wake wa facebook unaathiriwa na hisia zake."
Hata hivyo, utafiti huo umekosolewa kwa sababu watumizi wa Facebook hawakujuzwa kuwa walikuwa wakihusishwa.
Mbunge
wa chama cha Labour Jim Sheridan, mwanachama wa kamati ya uanahabari ya
Commons media select, ametoa wito kwa uchunguzi kufanywa kuhusu swala
hilo.
'Kuboresha taratibu zetu'
Kwa upande wake, Facebook imejitetea kwa kusema kuwa utafiti huo haukuhusisha ukusanyaji data wa watu usiohitajika."
"Hakuna data iliyotumiwa iliyohusiana na akaunti ya mtu yeyote maalum," ilisema Facebook
Siku ya Jumanne, bwana Allen alisema: "Sasa ni wazi kuwa watu walikasirishwa na utafiti huu na tumewajibika."
"Tunataka kufanya bora zaidi siku zijazo na kuboresha taratibu zetu kutokana na maoni haya."
Wakati
huo huo, Adam Kramer wa Facebook, ambaye pia alihusika katika kutoa
taarifa kuhusu uchunguzi huo , amekiri kuwa kampuni hiyo haikueleza
"vizuri nia yao katika ripoti yake."
"ninaelewa
ni kwa nini watu kadhaa wameonyesha hofu yao kuihusu, na waandishi
wenzangu pamoja nami tunaomba radhi kwa jinsi ambavyo ripoti ilieleza
utafiti huo pamoja na wasiwasi iliyosababishwa," alisema mapema wiki hii
No comments:
Post a Comment