Staa wa kitambo kwenye tasnia ya filamu za Kibongo, Stanley Msungu
MCHEPUKO? STAA wa kitambo
kwenye tasnia ya filamu za Kibongo, Stanley Msungu amenaswa laivu akiwa
kwenye pozi tata na mke wa mtu aliyetambulika kwa jina moja la Bonita.Tukio hilo lilijiri nje ya Mgahawa wa Great Wall uliopo Masaki jijini Dar, usiku wa saa saba ambapo kulikuwa na tafrija ya chakula cha usiku iliyoandaliwa na Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’.
“Dah! Kuna watu wana uhuru kweli na ndoa zao, yaani Bonita amefunga ndoa juzijuzi tu, mumewe amelala nyumbani yeye anahangaika huku na Msungu.
...akijificha kukwepa Kamera.
“Kama huamini nenda kwenye gari ukajionee wanachofanya Msungu na
Bonita au hadi tufanye sisi ndiyo mnatupiga picha?” alihoji mmoja wa
waigizaji walioalikwa kwenye hafla hiyo ambaye jina tunalihifadhi
akimsisitiza mwanahabari wetu kwenda kunasa tukio hilo.Mke wa mtu anayedaiwa kuchepuka na Stanley Msungu.
Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, Risasi Jumamosi kama kawaida yake lilinyata hadi lilipokuwa gari la Msungu kisha kunasa tukio hilo ambapo Bonita alikuwa akijificha asionekane vizuri huku Msungu akiwa katika hali ya kutaharuki.
“Kaka mke wa mtu huyu, utaniharibia mimi na yeye kwa mumewe, achana na hayo mambo kaka njoo tuzungumze,” alisema Msungu akijitetea huku Bonita akiomba kamera ya paparazi wetu iishe chaji ili zoezi la kupiga picha lisiendelee kabla ya kuondoka eneo hilo kwa spidi na kutaka kumgonga mwandishi.
No comments:
Post a Comment