BAADA ya kuibuka sintofahamu kati ya waigizaji wa
Bongo Movies, Salum Mchoma ‘Chiki’ na Vincent Kigosi ‘Ray’, Chiki
ameibuka na kuzungumzia ishu hiyo.
Akipiga stori mbili tatu na paparazi wetu, Chiki alisema kuwa yeye na
Ray hawakuwahi kuwa na bifu kama inavyozungumzwa kwenye mitandao ya
kijamii isipokuwa walipishana kauli kidogo katika bethidei ya muigizaji
Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’ iliyofanyika katika Hoteli ya Lamada, Ilala
jijini Dar lakini waliyamaliza.
“Sina bifu na Ray tuko poa, pale Lamada tulipishana maneno kidogo tu
ila kwa sasa stori kama kawa hatuna bifu la aina yoyote,” alisema Chiki.
Kwenye bethidei hiyo, ilidaiwa kuwa Chiki aliyekuwa MC wa shughuli
hiyo alimpa maneno ya ‘madongo’ kumsisitiza atoe mkwanja ‘fedha’ nyingi
kama zawadi kwa Dk. Cheni hali ambayo ilimuudhi Ray.
Imeandikwa na Maria Halimoja na Rhoda Josiah.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment