TUHUMA nzito ya aina yake ambayo haijawahi kutokea ambapo mkazi mmoja
wa Tandale – Kwatumbo wilayani Kinondoni jijini, Idd Mpenda anadaiwa
kumshambulia na kumjeruhi hadi kuzimia mkewe, Nasra Dafa (30) wakati
akiswali.
Akizungumza na Amani huku akimwaga machozi, mwanamke huyo alisema
tukio hilo lilijiri Julai 28, mwaka huu saa saba mchana wakati akiswali
maeneo ya duka lake lililopo Tandale.
ILIKUWA KUSHTUKIZA
Alidai kwamba alikuwa katika
kusujudu, mara mumewe alitokea na kumshambulia kwa mateke, ngumi na
viatu kisha akamburuza chini hadi nje hali iliyosababisha nguo aliyovaa
kuvuka na kubaki kama alivyozaliwa!“Kama unavyoniona, nimeumia sehemu
mbalimbali za mwili. Kiatu ndiyo kimeniumiza sana.
ATINGA KITUO CHA POLISI
Alisema baada ya tukio
hilo kutokea alijivuta na kuvaa gauni lingine kisha akakimbilia Kituo
Kidogo cha Polisi Tandale ambapo polisi walimwambia ishu yake ni nzito
na kumtaka aende Kituo cha Polisi Magomeni (vyote vipo Dar).
ASIMULIA VIPIGO, UKE WENZA
Mwanamke huyo aliweka
hadharani kwamba mumewe amekuwa akimpiga mara kwa mara na tatizo kubwa
ni uke wenza ambapo alidai ameoa mke wa pili hivi karibuni na mapenzi
baina yao yamezorota.
“Mimi kabla ya kufunga naye ndoa Januari Mosi, 2013 mume wangu
alikuwa na mke mwingine lakini aliamua kumpa talaka baada ya kumweleza
kuwa mimi sitaki kuwa mke mwenza.
“Tukawa tunaishi naye lakini hata hivyo hakuchukua muda mgogoro ukaanza ndani ya nyumba.
SAKATA LAFIKA KWA NDUGU
Mwanamke huyo aliendelea
kusema kwamba hali ilizidi kuwa mbaya hadi ikafika kwa wana ndugu kwa
suluhu, walipatanishwa lakini baada ya muda mgogoro ukaendelea na kuna
siku mumewe akamwambia ameoa mke mwingine wiki tatu nyuma.
SIKU YA TUKIO
“Siku ya tukio, nilikuwa naswali.
Unajua wakati wa Mfungo wa Ramadhani lazima Muislam kuswali kwa
kuzingatia taratibu zote za dini. Basi, alikuja na kuniita nitoke nje
lakini sikutoka.“Niliona nimalize kwanza kuswali ndipo nitoke, lakini
kabla sijamaliza akaja na kunishambulia kama niliovyokwambia kisha
akachukua funguo na kufunga duka.
“Alipotoka hapo akaenda kwenye duka lingine la kuuza vocha nalo
akalifunga na kuchukua fedha zote na kuondoka nazo huku muuzaji
akiambiwa aende kwake,” alisema mwanamke huyo.
Amani lilifika kwenye Kituo cha Polisi Magomeni na kuambiwa na askari
mmoja kuwa taarifa hizo zipo na mtuhumiwa anashikiliwa hapo, lakini
akashauri atafutwe Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP Camilius
Wambura kwa maelezo zaidi. Kamanda huyo hakupatikana ofisini kwake hadi
tunakwenda mtamboni.
SHEHE MKUU ASAKWA
Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Alhad Musa Salum hakupatikana kuzungumzia makosa ya mume wa
Kiislamu kumpiga mkewe wakati akiswali ndani ya Mwezi Mtukufu.Hata
hivyo, Maalim Hassan Yahya Hussein wa Magomeni Mwembechai alipoulizwa
alisema Uislamu haujatoa ruhusa kwa mwanaume kumpiga mkewe wakati
anaswali hata kama amefanya kosa kubwa kiasi gani.
“Uislamu haujaruhusu kwa hali yoyote udhalilishaji na kuna hadithi
zinazokataza mtu kumdhuru mwenzake. Kuna masharti sita yamewekwa kabla
ya mume kufikia hatua ya kumwadabisha mkewe,” alisema Maalim
Hassan.Akaendelea: “Kabla mume hajampa adhabu mke anapaswa kwanza kumpa
nasaha kwa kosa alilotenda na sharti la pili ni kumpa mawaidha ama yeye
mwenyewe au atafute mtu.
“Sharti la tatu ni kumkumbusha mara kwa mara na sharti la nne ni
kumhama malazi, yaani kumuacha alale peke yake. Sharti la tano, akikosa
ni kwenda kushitaki kwa wazee au katika vyombo vya sheria ikiwemo kwa
kadhi na viongozi wa dini.“Sita ndiyo kumpiga, lakini kipigo ambacho
hakitamdhuru kwani hutakiwi kumpiga ukiwa na hasira.”
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment