USIKU WA MATUMAINI 2014… HISTORIA KUANDIKWA UPYA


Rais Jakaya Kikwete akiwa na mpira tayari kuanzisha mechi ya wabunge wa Simba na Yanga wakati wa Tamasha la Usiku wa Matumaini 2013, mwaka huu linafanyika Agosti 8.
LILE tamasha lililokuwa likisubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki, linalotambulika kama Usiku wa Matumaini (Night of Hope), limewadia ambapo mwaka huu litafanyika Agosti 8 (Sikukuu ya Nanenane.)
Mashabiki wa timu ya Bongo Muvi wakiingia uwanjani kwa mbwembwe kabla ya timu yao kumenyana na Bongo Fleva mwaka jana.
Akizungumza na Mtandao huu, mratibu wa tamasha hilo, Luqman Maloto amesema mwaka huu wamelifanyia maboresho ya hali ya juu kutokana na kuchukua wasanii kutoka nje ya Afrika Mashariki ili kukata kiu ya Watanzania ambao walitoa maoni na kupendekeza aina ya wanamuziki na burudani wanazopenda ziwepo.
“Historia itaandikwa upya na kwamba Watanzania wakae tayari kuisubiri Agosti 8, mwaka huu, muda si mrefu tutaanza kutaja orodha kamili ya wasanii wakubwa tutakaokuwa nao ambao kwa hakika itakuwa ni sapraizi kwa mashabiki wa burudani Bongo,” alisema Maloto na kuongeza:
Dk. Jose Chameleone akifanya yake katika Tamasha la Usiku wa Matumaini 2012.
“Kama kawaida, Tamasha la Usiku wa Matumaini litafanyika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, ule mpya, mkubwa.”
Tamasha la Usiku wa Matumaini huandaliwa na Kampuni ya Global Publishers, ambapo linachukua nafasi kila mwaka na linawakutanisha watu wengi kutokana na matukio mbalimbali yanayolipamba tamasha hilo.
Benchi la timu ya Wabunge wa Simba.
Miongoni mwa matukio ambayo yalisisimua mwaka jana kwenye tamasha hilo ni pamoja na mechi za mpira wa miguu kati ya wabunge, ndondi za wabunge, mechi za Bongo Fleva na Bongo Movie, bendi mbalimbali kutumbuiza pamoja, mastaa mbalimbali wa muziki wa Gospo kutoka ndani na nje ya Bongo.

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger