SOO! Mtangazaji
anayedili zaidi na mambo ya haki za wanawake Bongo, Joyce Kiria
amenagwa na watu mbalimbali mitandaoni kwa kile kinachoonekana kuingilia
sakata la mwimbaji wa Injili nchini, Flora Mbasha na mumewe Emmanuel
Mbasha, akionekana zaidi kumtetea Flora.
Mmoja wa watoa maoni katika mtandao wake aliandika: “Joyce acha
kujidhalilisha, huoni kama unapoteza utu wako? Naanza kuamini kuwa na
wewe ni miongoni mwa wasioheshimu ndoa zao kutokana na kuwashauri
wenzako upumbavu!
“Kwa mantiki hiyo hustahili hata kuwepo kwenye Kipindi cha Wanawake
Live, ikiwa unatetea upumbavu. Acha kuingilia mambo yaliyopo mahakamani,
utapoteza mashabiki wako bure.”
Licha ya kunangwa kwa maneno makali mara kwa mara, Joyce ameendelea
kuandika kila wakati kuhusiana na ishu hiyo, akionyesha hisia zake
waziwazi kuwa yupo upande wa Flora jambo ambalo limepingwa vikali na
wachangiaji walio wengi, wakimtaka asijadili suala lililopo mahakamani.
No comments:
Post a Comment