STAA wa filamu Bongo, Wema Sepetu ametaja sababu
zinazomfanya aingie katika mgogoro na mama yake mzazi, Miriam Sepetu
kuwa ni suala la uchumba wake na Nasibu Abdul ‘Diamond’ ambao alikuwa
akiupinga mara kwa mara.
Akipiga stori na mapaparazi, Wema alisema kwa muda mrefu alikuwa
akitofautiana kauli na mama yake katika suala zima la uhusiano wake na
Diamond lakini anamshukuru Mungu amemuelewa na sasa kila kitu kinakwenda
sawa.
“Mama nilikuwa nikimsihi sana juu ya uchumba wangu na Diamond lakini
sasa tumefikia hatua nzuri namshukuru Mungu amekubali, maana siku hizi
nikionana naye ananiuliza vipi mwenzako mzima, anaendeleaje, wakati
mwanzoni haikuwa hivyo,” alisema Wema huku akiahidi kumkutanisha Diamond
na mama yake. Imeandikwa na Mayasa Mariwata na Shani Ramadhani
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment