HII ni exclusive! Kwa mara ya kwanza, staa
anayeitikisa nchi kwa sasa na wimbo wake wa Mwana, Ali Kiba amefunguka
kuwa mwigizaji kiwango Bongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ anafaa
kuwa mke (wife material) huku akiweka wazi sifa kibao alizonazo,
Wikienda liko bize kukujuza.
Kiba ambaye hivi karibuni ameibua mijadala mingi katika mitandao ya
kijamii, usafiri wa umma na kwenye baa juu ya ujio wake mpya akisemekana
kurudia kiti chake ambacho alikikalia Mbongo Fleva, Abdul Nasibu
‘Diamond’ kwa muda, mwaka 2010 aliwahi kuripotiwa katika magazeti pendwa
kwamba ana uhusiano wa kimapenzi na Lulu ambaye wakati huo alikuwa na
umri chini ya miaka 18!
LULU ANAFAA KUWA MKE
Akizungumza mbele ya kinasa
sauti cha Globa TV Online, Bamaga-Mwenge jijini Dar mwishoni mwa wiki
iliyopita, Kiba ambaye anatarajia kuangusha shoo ya kihistoria Agosti 8,
mwaka huu katika Tamasha la Usiku wa Matumaini kwenye Uwanja wa Taifa
jijini Dar, alisema Lulu anafaa kuwa mke kwa vile ni mchapakazi sifa
ambayo mke mwema anapaswa kuwa nayo.
AMMWAGIA SIFA
Kiba alisema Lulu anajua
kuhangaika, anajua kupambana kusaka pato lake kihalali kupitia mauzo ya
sinema zake anazozizalisha kitu ambacho kinawashinda mabinti wengi na
kuangukia katika biashara ya kuuza miili (ukahaba).
Licha ya kummwagia sifa hizo, kipindi hicho alichokuwa akitajwa kuwa
naye, Lulu alikuwa na matukio ambayo hayakuwa na maadili lakini Kiba
hayo hakuyatilia maanani.
Mwandishi: Unafikiri Lulu ni ‘wife material’ (mke mwema) ambaye unaweza kumweka ndani akalea watoto na kuijenga familia bora?
Kiba: Yeah! Anafaa kuwa mke, ni binti anayejituma, mchapakazi, mtafutaji. Kwangu mimi mtu wa namna hiyo ndiyo anafaa kuwa mke. Mwandishi: So, unataka kutuambia kwamba unaweza kumuoa? Kiba: Sijasema hivyo mimi, nimesema anafaa kuwa mke.
ACHOMOA KUBANWA KISHERIA
Licha ya kuchomoa ishu
hiyo ya uhusiano, mapaparazi wetu walimbana zaidi staa huyo afafanue kwa
nini alitajwa yeye na si msanii mwingine huku ikidaiwa kuwa, Lulu
hakuwa ametimiza miaka 18 hivyo kubanwa kisheria (ya watoto na
kujamiiana).
“Sijatembea naye ndiyo maana unaona hata sheria
haijanihukumu, endapo ningekuwa nimetembea naye, basi sheria ingeweza
kunitia hatiani na ningefungwa jela,” alifafanua Kiba.
AWASHANGAA WANAOMSHANGAA
Kiba aliongeza kuwa, anashangaa sana kuona watu wanamsema vibaya yeye kupendwa na Lulu.
“Lulu ni msanii mwenzangu, anapenda kazi zangu na mimi napenda za
kwake. Ni rafiki wa kawaida, hakuna kitu kingine cha ziada. Nawashangaa
wanaozusha ya kuzusha, hivi kwani kuna tatizo Lulu akinipenda? Sidhani
kama ni kosa, ana haki ya kunipenda kutokana na muziki wangu.
“Unajua muziki mzuri huwa unapenya automatically, huwezi kuzuia hisia
za muziki, mtu unaweza ukawa humpendi msanii f’lani lakini ukapenda
muziki wake, unajikuta tu unampenda, unaanza kuimba nyimbo zake,”
alisema Kiba.
KUMBUKUMBU MBICHI
Juzikati wakati Kiba
anatambulisha nyimbo zake mbili kwa mpigo (Mwana na Kimasomaso), Lulu,
kupitia mtandao wa Instagram alitupia maneno ya kummwagia sifa staa
huyo, liliibuka kundi ambalo linatajwa kuwa ni wafuasi wa mwigizaji Wema
Sepetu ‘Team Wema’ na kuanza kumshambulia kwa maneno machafu.
KIBA AFUNGUKA
Akizungumzia ishu hiyo, Kiba
alisema waliofanya hivyo hawakumtendea haki Lulu kwani ana haki ya
kueleza hisia zake pale anapoguswa na muziki mzuri.
“Hawajatenda haki kwa sababu Lulu ni binadamu kama walivyo wengine, ana haki ya kupenda kitu kizuri,” alisema Kiba.
KUHUSU KIFO CHA KANUMBA
Kiba akizungumzia juu ya
kuhusishwa na kifo cha aliyekuwa nyota wa sinema Bongo, marehemu Steven
Kanumba ambapo alidaiwa kunaswa kwa meseji za mapenzi alizozituma kwa
Lulu ndiyo zilizosababisha mtifuano ambao ulisababisha kifo cha Kanumba,
alikana madai hayo.
“Si kweli, sikuwa nimewasiliana na Lulu siku hiyo kabla ya tukio.
Nakumbuka nilikuwa safarini, baada ya tukio nilimpigia Lulu kutaka kujua
ukweli wa taarifa za kifo kwa sababu marehemu alikuwa mtu wangu wa
karibu kama alivyo Lulu,” alisema Kiba.
AMGUSIA WOLPER
Kwenye mahojiano hayo, mkali huyo
alizungumzia ishu ya mwigizaji, Jacqueline Wolper kukiri kwamba Kiba
ndiye mwanaume aliyemtoa usichana wake kwenye simulizi iliyochapishwa
katika Gazeti la Championi hivi karibuni.
“Mh! Aliwahi kukiri? Daah! Sijui bwana… Wolper ni mtu wangu wa karibu
kama alivyo Lulu,” alisema kwa mkato Kiba.Juzi, Lulu alitafutwa na
mapaparazi wetu ili azungumzie ukaribu wake na Kiba, lakini simu yake
muda mwingi iliita bila kupokelewa (tunaamini atasoma hapa, tunaendelea
kumtafuta ili afunguke).
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment