KAULI ya nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kwamba hawezi kuoa kamwe, inadaiwa kumchefua mwandani wake, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’, Amani limenyetishiwa.
Aliporejea Bongo kutoka Marekani juzikati, Diamond alitoa kauli hiyo na kuandikwa kwenye ukurasa wa mbele wa gazeti dada la hili, Ijumaa, toleo la wiki iliyopita likiwa na kichwa cha habari; ‘DIAMOND: SITAOA KAMWE’ ambapo ndani yake alieleza jinsi ambavyo mastaa wengi waliooa wameanguka kisanii. MTU WA KARIBU AYASEMA YA WEMA
Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa mastaa hao, Wema hakufurahishwa na habari hiyo kwa sababu anajua yeye ndiye mke mtarajiwa wa Diamond.
Ilidaiwa kwamba, Wema alijikuta akipoteza ile furaha ya kwamba wawili hao wangefunga ndoa mwezi huu (Agosti) kama ilivyotabiriwa na mnajimu maarufu Bongo, Maalim Hassan Yahya Hussein.
Staa Nasibu Abdul ‘Diamond’ akiwa kwenye pozi lenye utata.
“Baada ya kauli hiyo ya Diamond na kutotimia kwa utabiri wa Maalim Hassan kwa sababu hakuna hata dalili za maandalizi ya tukio hilo muhimu kwenye maisha ya mwanadamu, Wema ameanza kukata tamaa, lakini amesema hawezi kulazimisha ndoa kwa mwanaume kwa kuwa si utamaduni wa wanawake wa Kitanzania wala Kiafrika.
“Unajua Kibongobongo au hata Kiafrika hai-sound vizuri na pengine haiwezekani kwa mwanamke kulazimisha kuolewa kama mwanaume hataki. Hicho ndicho kilichomtibua Madam (Wema) baada ya kusoma alichokisema Diamond,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:
“Wema amehisi yeye ni girl lover (mpenzi) tu kwa Diamond na si wife material (mke mwema) kwa hiyo anawaza sana kuhusiana na ishu hiyo japo mahaba niue kati yao yanaendelea, lakini anafikiria kuchukua uamuzi mzito.”
WEMA SASA
Baada ya kuinyaka ishu hiyo, gazeti hili lilimtafuta mlimbwende huyo anayeshikilia Krauni ya Miss Tanzania 2006 ili kumsikia mwenyewe ambapo alifunguka yake ya moyoni.
Mwanadada huyo alisema kuwa kwa sasa haumizi tena kichwa kuhusu suala la ndoa na Diamond na kwamba hana haraka nalo.
“Mimi naamini sana mambo ya utabiri, lakini siumizi kichwa na suala la kuolewa na Diamond na kamwe siwezi kumlazimisha anioe.
Aliporejea Bongo kutoka Marekani juzikati, Diamond alitoa kauli hiyo na kuandikwa kwenye ukurasa wa mbele wa gazeti dada la hili, Ijumaa, toleo la wiki iliyopita likiwa na kichwa cha habari;
‘DIAMOND: SITAOA KAMWE’
ambapo ndani yake alieleza jinsi ambavyo mastaa wengi waliooa wameanguka kisanii.
MTU WA KARIBU AYASEMA YA WEMA
Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa mastaa hao, Wema hakufurahishwa na habari hiyo kwa sababu anajua yeye ndiye mke mtarajiwa wa Diamond.
Ilidaiwa kwamba, Wema alijikuta akipoteza ile furaha ya kwamba wawili hao wangefunga ndoa mwezi huu (Agosti) kama ilivyotabiriwa na mnajimu maarufu Bongo, Maalim Hassan Yahya Hussein.
“Baada ya kauli hiyo ya Diamond na kutotimia kwa utabiri wa Maalim Hassan kwa sababu hakuna hata dalili za maandalizi ya tukio hilo muhimu kwenye maisha ya mwanadamu, Wema ameanza kukata tamaa, lakini amesema hawezi kulazimisha ndoa kwa mwanaume kwa kuwa si utamaduni wa wanawake wa Kitanzania wala Kiafrika.
“Kikubwa katika mapenzi ni upendo wa kweli ambao ananionesha bila kipimo. Wala sina papara, hata kama mtabiri kasema ndoa yetu ni lazima ifungwe mwaka unaogawanyika kwa mbili kwa maana ya mwaka 2016 kama itashindikana mwezi huu, hilo kwangu si tatizo la kunifanya nililie kuolewa na Chibu (Diamond).
“Ninachojua mimi Mungu ndiye anapanga yote na kama ndoa ipo ipo tu maana kuna watu wapo kwenye ndoa na hawana upendo wa kweli kama tulionano sisi,” alisema Wema. MAMA WEMA ANASEMAJE?
Paparazi wetu alimtwangia simu mama yake Wema, Mariam Sepetu na kumuuliza mambo mawili, kuhusu bintiye kuvishwa pete ya ndoa na Diamond na suala la Mbongo Fleva huyo kusema hataoa kamwe!
“Mimi niseme nini? Sina la kusema kuhusu Wema. Mambo yake ni yake mwenyewe na huyo Diamond wake. Kwanza kwa nini mnipigie mimi, si mumtafute yeye mwenyewe?” alisema mama huyo kwa sauti ya utulivu. MAMA DIAMOND AFUATA NYAYO
Katika hali ya kushangaza, mama Diamond, Sanura Kasim ‘Sandra’ ameonekana kunawa mikono kwa kauli aliyowahi kuitoa siku za nyuma kuhusu mtoto wake na masuala ya kutooa au kuoa.
Nasibu ni mtu mzima sasa, siwezi kumpangia lolote kuhusu kuoa au kutooa. Wakati ukifika, anaweza kusema lolote ambalo ataliona ni zuri katika maisha yake.” KUHUSU PETE YA NDOA
Kuhusu Diamond kumvisha pete ya ndoa Wema, tendo ambalo lilifanyika hivi karibuni wakiwa nchini Afrika Kusini, Amani lilifanikiwa kuzungumza na shehe mmoja ambaye aliomba hifadhi ya jina lake ambapo alisema alichokifanya Diamond kwa Wema ni usanii.
“Diamond amemfanyia usanii mwenzake. Pete gani bila kufunga ndoa. Halafu katika Uislam, hakuna tendo la wanandoa kuvalishana pete, hayo mambo wanayafanya wenyewe, ” alisema shehe huyo. WEMA AIZUNGUMZIA PETE
Wema alipopewa nafasi ya kuizungumzia pete hiyo alisema Diamond aliipenda tu akaamua kumnunulia na kumvisha lakini haihusiani na ndoa.
“Sisi (na Diamond) tulikuwa Afrika Kusini, baby wangu akaipenda pete, akainunua na kunivalisha, haina uhusiano na ndoa,” alisema Wema.

No comments:
Post a Comment