Zimemtembelea! Prizenta wa Kipindi cha Mitikisiko ya
Pwani kinachorushwa na Radio Times FM, Hadija Shaibu ‘Dida’ ameonesha
jeuri nyingine ya fedha baada ya kununua magari mengine mawili kwa
mpigo.
Dida amefanya kufuru hiyo ikiwa imepita miezi kadhaa tangu atangaze
kuwa ana nyumba mbili maeneo ya Goba na Kigamboni pamoja na kuyaanika
magari manne anayomiliki (Toyota Verossa mbili, Toyota Noah nyeusi na
Toyota Vitz.)
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, rafiki wa karibu wa Dida aliyeomba
hifadhi ya jina alisema ameshtushwa na kitendo cha shosti wake huyo
kununua magari mawili kwa mpigo kiasi cha kumfanya ahisi kuna biashara
nyingine anaifanya tofauti na utangazaji.
“Kanunua magari mawili, Toyota Noah na Toyota Brevis New Model. Yaani
hata sisi mashosti zake anatufanya tuhisi labda anafanya ile biashara
ya unga kama watu wanavyohisi.
“Ni kweli anafanya biashara zake lakini ndiyo apate fedha za kuonesha
jeuri hiyo? Ila kama ni kupambana na maisha, sasa hivi anapambana
kikwelikweli, hata akijiita Boss Lady ni sahihi kabisa,” alisema mtoa
habari huyo.
Baada ya kupata taarifa hizo, mwandishi wetu alimtafuta Dida ili kujua ukweli wa magari hayo, alipopatikana alifunguka:
“Siwezi kujiita Boss Lady kimdomomdomo tu, huwa napenda kufanya kitu
watu ndiyo waseme, nimeongeza magari mengine mawili. Moja ni Noah kwa
ajili ya biashara zangu na lingine ni Toyota Brevis la kutembelea,”
alisema Dida aliyetengana na mumewe, Ezden Jumanne siku chache
zilizopita.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment