MSHANGAO! Baadhi ya wasanii wa Klabu ya Bongo
Movie Unity wamejikuta wakipigwa butwaa baada ya kutinga nyumbani kwa
staa mwenzao, Devota Mbaga ambaye ni katibu wa klabu hiyo na kukuta
akiishi maisha ya kifahari.
Akipiga stori na gazeti hili, mmoja wa wasanii ambao walitia timu
nyumbani kwa msanii huyo, Kigamboni, Dar ambaye hakuwa tayari jina lake
lichorwe gazetini alisema, ilikuwa ni kama maajabu kwao kwa kukuta
nyumba ya kifahari na kujua miradi yake mbalimbali lakini haringi.
“Kusema ukweli tumeshtuka, hatukutegemea kabisa, tulijua maisha yake
ni ya kawaida, maana siyo mtu wa kujivuna kama wengine wenye nazo,
nahisi kwa maisha aliyonayo sidhani kama yupo mdada wa Bongo Movie
anayempata kwa utajiri alionao,” alisema msanii huyo.
Alipoulizwa Devota kuhusu ishu hiyo, aliishia kuangua kicheko na
kusema mafanikio yake hayatokani na shughuli za sanaa pekee bali
anajihusisha na miradi mbalimbali.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment