HUYU ANAOMBA USHOSTI
Maimartha wewe ni mtangazaji mzuri wa Bongo, naomba uwe shosti wangu wa kubadilishana mawazo. Salim Liundi, Dar, 0659601205
MAIMARTHA: Asante, kuhusu kuwa shosti, karibu sana hamna shida.
ALIANZA LINI UTANGAZAJI?
Ni wazi kabisa wewe ni
nguli katika tasnia ya utangazaji ila napenda kufahamu ulianza lini fani
ya utangazaji? Amiri Salumu, Dar, 0653252416
MAIMARTHA: Utangazaji nilianza miaka tisa iliyopita.
KABILA
Kwanza nakupa pongezi kwa kutokuwa na
skendo, mimi nataka kujua wewe ni kabila gani na ni mzaliwa wa mkoa
gani? Selemani Alifa, Dar, 0718803204
MAIMARTHA: Kabila langu ni Mchaga na nimezaliwa Morogoro.
HISTORIA
Mambo mumy, ningependa kujua historia yako kwa ufupi. Msomaji, 0712611705
MAIMARTHA: Mimi ni mtoto wa sita kati ya saba tuliozaliwa katika
familia yetu, nina elimu ya kidato cha nne na chuo cha uandishi wa
habari na utangazaji.
ANAUZA DAWA?
Hivi ni kweli dada Maimartha ulimsuta Sajo kwa ajili ya umbeya wake na
kweli dukani kwako una dawa za kuongeza makalio? Msomaji, 0713455487
MAIMARTHA: Ni kweli nilimsuta Sajo lakini siyo kwa roho mbaya ila
nilitaka tu aache umbeya, kuhusu dawa njoo dukani kwangu kwa maelezo
zaidi.
HUYU ANATAKA KUJUA
Je, Maimartha umeolewa na una watoto dada yangu? Gerald Soso, Dar, 0713565435
MAIMARTHA: Nimeolewa na nina watoto.
VIPI KUHUSU KINYAIYA
Ule umoja na Kinyaiya (Ben) bado upo? Mallya, Moshi, 0787978702
MAIMARTHA: Umoja upo mpaka sasa kwa sababu Kinyaiya ni kaka yangu.
DARAJA LA USTAA
Nakupongeza kwa kuwa MC
(mshereheshaji) mzuri na mzoefu. Je, wewe binafsi unajiweka kwenye
daraja gani la ustaa? Prince Dulla, Dom, 0758327997
MAIMARTHA: Ustaa
wangu ni wa kawaida tu, ninamheshimu kila mtu ila niko kwenye daraja la
kwanza kwa sababu mimi ni binti mwenye maadili ya Kitanzania.
ANA MGANGA WAKE?
Mimi nakufahamu vizuri
Maimartha na mimi ndiye niliyekufanyia mpango wa kukutoa katika
utangazaji lakini usilolijua ni sawa na usiku wa giza, umetoka kimaisha
hutaki kunisikia, simu yangu hupokei ila mimi ni mganga wako
nilikusaidia sana. Mr Kapaula, Dar, 0716941832
MAIMARTHA: Mimi mganga wangu ni Yesu tu, sikufahamu.
KUHUSU KUMSUTA SAJO
Dada Maimartha nina swali
dogo kwako, hivi uliwaza nini mpaka mkaenda kumsuta kijana wa watu Sajo,
unavyoona lilikuwa jambo la busara na haki kwa mtoto wa kiume? Tafakari
kabla ya kutenda. Abuu Sungura, Dar, 0654799098
MAIMARTHA: Siku
hizi kina mama wengi wanawasuta watu kwa matusi lakini mimi niliona ni
vyema nimnunulie keki na shampeni na ni kwa nia nzuri tu ili
kutojishushia heshima katika jamii.
ALIWAHI KUWA NA WAPENZI WANGAPI?
Mimi napenda kujua kabla ya kuwa na mume wako uliwahi kutoka na wapenzi
wangapi na kwa nini ulimtosa marehemu P.Didy? Chiku Ashery, Tanga,
0712791665
MAIMARTHA: Namheshimu mume wangu na wakwe zangu hivyo siwezi kuzungumzia mambo yaliyopita.
HUYU ANAHOJI
Nakupa hongera kwa kazi nzuri ila napenda kufahamu una elimu gani? Diana John, Tarime, 0762618265
MAIMARTHA: Nina elimu ya kidato cha nne na cheti cha uandishi wa habari na utangazaji.
MBONA KIMYA?
Eti dada yangu una mtoto mmoja au una wengine nje? Halafu siku hizi huvumi sana au ndiyo unaiheshimu ndoa? Msomaji, 0659528785
MAIMARTHA: Naona umejijibu mwenyewe, ni kweli nina watoto wengine ambao
ni wa mume wangu, nawapenda sana, kuhusu kuvuma ni kwamba nimeshaolewa
lazima nijiheshimu.
KUVAA KIMINI MSIBANI
Hivi ulipokuja pale Leaders kwenye msiba wa Kuambiana na kile kinguo ulikuwa umetoka klabu? Fariji Yusuph, Dar, 0762600630 MAIMARTHA:
Nilitokea kwenye uandaaji wa vipindi vyangu vya tv hivyo nikaona ni
vyema nikamsindikize mwenzangu katika safari yake ya mwisho.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment