NENO! Mwigizaji wa kitambo
Bongo, Suzan Lewis ‘Natasha’ amewataka wasanii wenzake kuachana na
tabia ya kuingiza ustaa kwenye ndoa, jambo ambalo linasababisha kuwa na
sifa mbaya ya kutodumu kwenye ndoa.
Akichonga na mwanahari wetu, Natasha alisema kuwa sababu ya ndoa za
mastaa wengi kuvunjika ni kutokana na kujiona wao wako juu na kushindwa
kuheshimu ndoa huku wakiwaona waume zao ni kitu cha kawaida.“Mastaa mkishaingia kwenye ndoa wekeni ustaa pembeni, muwe na heshima ili tuweze kufuta dhana iliyojengeka kwa jamii kwamba ndoa za mastaa hazidumu,” alisema Natasha ambaye amedumu kwenye ndoa kwa takriban mwaka mmoja sasa.
No comments:
Post a Comment