NI
laana! Baadhi ya mastaa wamenaswa laivu wakifanya vitendo
vilivyotafsiriwa kuwa vya kifuska, Ijumaa Wikienda lina mkanda kamili.
Baadhi ya mastaa wakionyeshana ufundi wa kucheza.
Tukio
hilo lilijiri kwenye Ukumbi wa Letasi Lounge uliopo maeneo ya Victoria,
Dar wikiendi iliyopita ambapo kulikuwa na Kibao Kata cha mtoto wa
mjini, Rose Alphonce Nungu ‘Muna Love’.
...Burudani baada ya kukolea, hali ilikuwa hivi.
Ndani
ya ukumbi huo lilishuhudia laana za aina yake ambazo zilikuwa
zikiongozwa na mwenye shughuli ambaye alikuwa akikata mauno ya ajabu kwa
staili ya ‘baba na mama’ chumbani.
Husna Maulid akionyesha ufundi.
“Duh!
Yaani utafikiri watu hawajui kuwa hii ni Kwaresma, ni full laana hebu
angalia Husna Maulid, Sajent (Husna Idd) na Davina (Halima Yahya)
wakiongozwa na Muna wanavyojichetua hadi ‘makufuli’ yanaonekana,”
alisema mwanadada mmoja.
Husna Idd 'Sajent' naye akionyesha machejo yake.
Katika
hatua nyingine, mwanaume tata anayejulikana kwa jina la Agrey alivua
nguo na kubaki na ‘kufuli’ kisha alipanda juu ya kiti na kuanza kuonesha
staili mbalimbali za ukataji wa mauno.
“Tobaa… jamani mwangalieni Agrey, kavua nguo anamwaga radhi…hahahaaa,” alisikika msanii mmoja wa Kundi la Vituko Show.
...Sajent na Husna wakizidi kujiachia.
Kingine
kilichojiri ni pale shindano lisilokuwa rasmi la kuzungusha nyonga
lilipoibuka kati ya watoto wa Ilala linaloongozwa na Baby Tunu na Baby
Tau ambao walishindana na watoto wa Kinondoni, Sajenti na wenzake, hali
iliyosababisha watu kushindwa kuvumilia na kuinuka vitini.Ili kunusuru hali, mshereheshaji wa shughuli hiyo, Chumi Suleiman ‘Bi Hindu’ alilazimika kuzima muziki kuepusha laana iliyokuwa inazidi kuvuka mipaka.
No comments:
Post a Comment