Staa wa filamu za Kibongo asiyekaukiwa na vituko, Aunt Ezekiel (katikati) akiwa karibu na dansa wa Wasafi Classic, Moses Yobo.
Aunt alinaswa akiwa na mnenguaji wa Wasafi Classic, Moses Yobo
anayepiga mzigo chini ya Nasib Abdul ‘Diamond’ katika shoo ya Fiesta
iliyofanyika jijini hapa katika Uwanja wa CCM Kirumba, wikiendi
iliyopita.Awali, katika gazeti hili, toleo la wiki iliyopita, tuliripoti habari ya Aunt kufanyiwa vurugu nyumbani kwa Wema na mke wa Yobo aliyekuwa na timu yake.
Baada ya habari hiyo kutoka, Aunt aliibuka na kusema kuwa, hana uhusiano wa kimapenzi na Yobo lakini kwa sababu amezushiwa, akaahidi kujiweka karibu na kumfanyia mitego ili atoke naye kweli ndipo afanyiwe vurugu ya halali.
Kuonekana akiwa naye jijini Mwanza, tena kwa ukaribu kama wapenzi huku wawili hao kila mmoja akiwa hana mpenzi wake anayetambulika, kulitafsiri kuwa Aunt ameamua kukinukisha.Habari ambazo Risasi Mchanganyiko halijazithibitisha kutoka kwa watu wa karibu na Aunt, zinasema kuwa, usiku huo baada ya shoo, wawili hao walilala pamoja katika hoteli ambayo haijajulikana.
Paparazi wetu baada ya kuona hali na ukaribu huo alimfuata Aunt ili kujua kama kweli ameamua kutekeleza azma aliyoitangaza, lakini akaruka kimanga.
“Nimeamua kukaa na Yobo karibu ili kuwazingua wasanii ambao baada ya kuniona wakawa wananitania eti mimi mkewe kutokana na taarifa za magazeti zilizoripotiwa hivi karibuni, ila ukweli mwenyewe unaona tupo hapa na Wema (Sepetu) na watu wengine na kimsingi hakuna kitu kibaya kinachoendelea kati yetu,” alisema Aunt.
No comments:
Post a Comment