MAAJABU: BABA WA FAMILIA AJIFUNGUA MTOTO
Familia inayoundwa na wanandoa Bianca na Nick Bowser, ni familia yenye furaha lakini iliyowashangaza wengi baada ya Nick ( baba wa familia) kupata ujauzito na kujifungua.
Iko hivi; Nick ambaye ana umri wa miaka 27 hivi sasa, alizaliwa na jinsia ya kike na kupewa jina la Nicole na wazazi wake, lakini aliamua kubadilika na kuishi kama mwanaume (transgender/jike dume) tangu miaka saba iliyopita. Na hii ilichangiwa pia na sura na umbo la kiume alilokuwa nalo.
Hali ilikuwa hivyo pia kwa Bianca ambaye ana umri wa miaka 32 hivi sasa, yeye alizaliwa mwanaume na kuitwa jina la Jason, lakini kutokana na kuwa na sura nzuri na umbo la kike, na hisia zake za kutaka kuishi kama mwanamke, alibadili aina ya maisha na kuishi kama mwanamke kamili.
Wawili hao walikutana na kuamua kufunga ndoa huku wakiyabadilisha kabisa maisha ya wana ndoa, Nick akiwa baba wa familia anaevaa na kuishi kama mwanaume. Mkewe Bianca (ambaye ni mwanaume) yeye alibadili na kuishi kama mwanamke kamili akiihudumia familia yake na kuvaa mavazi ya kike kama mama siku zote.SOMA ZAIDI>>
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment