July 25, mwaka huu, Ali Kiba alivunja ukimya wa muda mrefu kwa kuachia nyimbo mbili kwa mpigo ambazo ni ‘Mwana Dar es Salaam na Kimasomaso’. Wengi walisubiri kwa hamu ujio wake mpya na waone kama kweli atatusua au itabuma!
Bila
shaka yeye pia alikuwa na tension kujua jinsi gani nyimbo hizo
zitakavyopokelewa na mashabiki hao. Je wazikubali sana au wataona
kawaangusha?
Ripoti
zilizonaswa na tovuti ya Times Fm kupitia vyanzo mbalimbali vikiwa ni
pamoja na baadhi ya ma DJ wanaofanya kazi Times Fm Radio na katika club
mbalimbali zinaonesha kuwa Mwana Dar es Salaam inafanya vizuri sana hasa
club.
“Aisee,
kwa kweli nimepiga club kadhaa na kuhudhuria club karibia zote kubwa za
mjini. Nimegundua wimbo wa Ali Kiba, Mwana Dar es Salaam unafanya
vizuri sana. Kiukweli inafanya vizuri sana hasa kwa kulinganisha na muda
ulioingia sokoni. Yaani ukiupiga unaona watu wanakuelewa kibao aisee.”
DJ ambaye hakutaka jina lake litajwe ameiambia tovuti ya Times Fm.
DJ
mwingine ambaye alikubaliana na maelezo ya DJ wa kwanza kuhusu wimbo wa
Ali Kiba, aliongeza kuwa bado wimbo wa Diamond, Mdogo Mdogo ndio wimbo
ambao anaweza kuutaja kama wimbo wa kuwaamsha watu zaidi.
“Ukitaka
club pavurugike. Yaani watu wafurike kwenye dance floor kwa fujo… we
piga tu MdogoMdogo ya Diamond. Yaani haielezeki shangwe yake aisee. Watu
wanapagawa.” Alisema.
Nyimbo
zote mbili zinapata nafasi nzuri sana katika vituo vya radio.
MdogoMdogo ambayo ina video ya kimataifa inachezwa sana na kukubalika
kwenye vituo vya mbalimbali vya runinga. Youtube, video hiyo
imeshaangaliwa zaidi ya mara 717,000 kwenye akaunti ya Diamond pekee.
Mashabiki wengi wana kiu ya kuiona video ya wimbo wa Ali Kiba ambayo inabidi iwe na level kubwa kulingana na wimbo wenyewe.
Wimbo
wa Diamond ‘Mdogo Mdogo’ ulitoka rasmi June 12, baada ya mwezi mmoja na
wiki moja ukatoka wimbo wa Ali Kiba ‘Mwana Dar es Salaam’.
No comments:
Post a Comment