Msanii aliyewahi kutamba miaka ya nyuma na kundi la Kaole Nuro Nassoro 'Nora' ameamua kufunguka baada ya tuhuma nzito iliyokuwa inamkabili ya kudaiwa kuchoropoa mimba ya msanii mwenzake.....
Nora
anadaiwa kuwa katika uhusiano na mmoja wa wasanii wa siku
nyingi huku wiki za hivi karibuni akifululiza kwenda hospitali
na wambeya wakadai ni ujauzito na kwamba yupo kwenye harakati
za kuutoa...
Nora
mwenyewe akiongea na mwandishi wa habari hii aliweka wazi
kuwa suala la kwenda hospitali kupima ni kawaida yake na
kwamba maneno hayo yanakuzwa na wabaya wake....
"Hakuna
suala kama hilo. Hivi mtu kwenda kucheki afya yako ndo kutoa
mimba? mbona wapo wanaokesha huko na hawasemwi? Sina mpango huo
na huyo msanii anayejitapa kuwa nimetoa mimba yake nikimjua
atanieleza ni lini nililala naye mpaka akanipa mimba",alisema Nora
No comments:
Post a Comment