Kumekuwa na msisimko mkubwa katika vyombo vya habari na mitandao ya
kijamii nchini Kenya kuhusu taarifa ya msichana wa Kihindi aliyekiuka
mila na tamaduni za jamii yake na kuolewa na kijana Mwafrika.
Msichana huyu wa kihindi anaitwa Sarika Patel, na ameolewa na kijana wa
kabila la Bukusu Timothy Khamala, jambo ambalo ni nadra sana kwa watu wa
jamii ya kihindi. Kilichowashangaza wengi ni kwamba Sarika ametoka
katika familia tajiri na kuamua kuishi maisha ya walalahoi kijijini
Kwa Sarika maisha ya umaskini ambayo Timothy anaishi sio kikwazo hata
kidogo bali kwake hapo ndipo anapata raha na mapenzi ambayo anasema
yamemridhisha na kumtuliza nyumbani kwa kijana Timothy.
Timothy alikuwa anafanya kazi nyumbani kwa kina Sarika kama mjakazi
lakini akafutwa kazi na baba ya Sarika baada ya kupendana na msichana
wake.Kwa sasa yeye ni tarishi katika ofisi hii ya jimbo.Sarika hana
kazi
Wawili hao sasa wapo katika pilka pilka za kuanza maisha mapya ila kwa
pingamizi kali . Sarika Patel anasema kulingana na mila yao si sawa
kuolewa na mtu asiyekubaliwa au kuchaguliwa na wawazi wako. Wachumba kwa
kawaida hutoka jamii sawa.
Mbali na tofauti ya rangi zao za ngozi , Sarika anatoka katika familia
tajiri kinyume na mumewe Timothy ambaye ni mlalahoi. Licha ya tofauti
hiyo, Sarika anasema wazazi wake hawangeweza kumzuia kumpenda amtakaye
No comments:
Post a Comment