Kuna watu ambao wamekuwa hodari kujisifu kuwa wao hutoa unyumba kwa
‘kibaba’. Yaani huwapimia wenzi wao. Kwa mitazamo yao, hujiona wapo
sahihi. Tabia hii ipo kwa wanawake zaidi, japo kuna wanaume ambao nao ni
wagumu kutekeleza mahitaji ya wapenzi wao.Hata hivyo, kuna kitu cha
kuweka sawa hapa; Wakati mwanamke anapobana ‘staftahi’ kwa mwenzake,
huhesabika ni mchoyo! Kwa mwanaume yeye huonekana ni goigoi. Kwamba
mambo hayawezi ndiyo maana hatekelezi shughuli. Ataambiwa ana tatizo la
zile nguvu zetu!
Mwanamke anaweza kujisifu hata kwa wenzake. Akiwa kwenye vikao vya
kusukana au katika soga nyingine, atajimwagia sifa tele kwamba yeye
inaweza kupita miezi bila kuingia uwanjani na mwenzi wake. Hili,
linawafanya wanaume wengi wateseke na matokeo yake hutafuta tiba
mbadala.
Mwanaume hawezi kujisifu kwa marafiki zake kuwa yeye huwa akisumbuliwa
na mwenzi wake, humpa mgongo! Ni wazi akisema hivyo atachekwa. Yaani
mwanamke kugomea kutoa unyumba ni ushujaa wakati mwanaume akikataa,
atachukuliwa kwamba ana tatizo la kiafya! Dhana hii sikubaliani nayo,
kwa hiyo nahitaji kutoa shule!Kwangu mimi, kila aliye mvivu wa kuingia
shughulini ana tatizo! Kwa mwanaume na mwanamke, wote wana kasoro ya
nguvu, kwa maana hiyo wanahitaji tiba mbadala ili waweze kusherehekea
tendo. Wanatakiwa kuboresha mvuto wao katika ndoa au uhusiano na nafasi
ya kutekeleza hilo ipo!Ni lazima watu waheshimu uhusiano wao wa
kimapenzi. Pia waelewe kwamba moja kati ya vitu vinavyoshikilia penzi
lako ni unyumba. Ni wakati muafaka kwako sasa, kuachana na mawazo ya
kale. Punguza uvivu na ujue kuwajibika inavyotakiwa, kwa maana ni njia
ya kutibu amani yako mwenyewe na mwenzio.
Utafiti unaonesha kwamba asilimia kubwa ya ndoa zinazovurugika kila
siku, nyuma yake huwa na shambulio la wanandoa kutopeana huduma ya
tendo. Kwamba, wanavumiliana lakini mwisho wa siku, sauti itasikika kwa
majirani. Watakapokuwa wanagombezana usiku, siri hugeuka sirini.
Tendo la ndoa, hukamilisha furaha ya wawili walioamua kupendana.
Tunapoamua kuacha siasa na kuzingatia ukweli kwa vipimo vyake, watu
wengi (hasa wanaume), wanapoingia kwenye uhusiano wa kimapenzi, lengo
lao la kwanza ni kutimiza haja zao kimwili kwa mtu husika. Nazungumza
kwa utafiti!
Walikutana barabarani, akavutiwa ndiyo maana akaanza misele.
Anapofanikiwa, vikwazo vya baadaye, inakuwa siyo matarajio yake.
Alichotarajia ni kwamba baada ya kukubaliana kuingia kwenye sehemu yenu
‘spesho’, atakuwa hapimiwi! Kwa kiwango chochote atakachokuhitaji,
mwenzi wake atamridhia.
Aghalabu, wapenzi ambao wanajikuta wapo kwenye mgogoro wa tendo, mara
nyingi hukabiliwa na tatizo la usaliti. Ni theluthi moja ya wanawake
wanaoweza kumvumilia mwanaume ambaye hamtoshelezi kimwili, wakati kwa
wanaume ni moja ya kumi tu ndiyo wenye kuvuta subira hadi siku
watakapokumbukwa.
“Huyu mbona yupo hivi, kila siku anasema kachoka, atakuwa ana mtu huko
nje,” ni kauli ambayo ni rahisi kupita kichwani kwa mwanamke, pale
ambapo anakabiliana na mwenzi ambaye haguswi chochote na tamaa za mwili,
ingawa inaelezwa kwamba ni moja ya kumi ya wanawake ndiyo hukosa
usingizi kwa kunyimwa tendo.
No comments:
Post a Comment