WEMA ATOA DAU LA MILIONI ATAKAYEMUONA MBWA WAKE, SOMA ZAIDI HAPA

BEAUTIFUL Onyinye, Wema Sepetu ametangaza dau la shilingi milioni moja kwa yeyote atakayefanikisha kupatikana kwa mbwa wake aitwae Vanila aliyepotea hivi karibuni.
Beautiful Onyinye, Wema Sepetu.
Akielezea ishu hiyo, Wema alisema mbwa huyo alikuwa na mwenzake akiishi nao nyumbani kwake Kijitonyama jijini Dar es Salaam ambapo juzikati alikorofishana na mwenzake aitwae Thiona na kuamua kutokomea kusikojulikana.
Mbwa wa Wema Sepetu aitwae Vanila.
Msanii huyo alisema anaomba yeyote atakayemuona Vanila wake awasiliane naye au atoe taarifa kituo chochote cha polisi kilicho karibu naye na atakabidhiwa pesa zake taslimu.

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger