YOUNG KILLER APIGWA HADI KUZIMIA ALIPOGUNDULIKA TU ANAFANYA MUZIKI,

Mama wa msanii wa muziki wa Hip Hop Young Killer Msodoki, amesema kuwa anafurahishwa sana na kipaji cha mtoto wake ambacho kinaendelea kuonekana siku hadi siku licha ya kwamba mwanzoni aliwahi kumkataza kwa kumpiga mwanaye huyo mpaka kuzimia ile aachane na muziki. 


Young Killer akiwa na mama yake 

Mama Msodoki alikuwa akizungumza na Bongo5 jana jijini Mwanza. 

“Kwanza namshukuru Mungu kwa kufanya mwanangu kufikia hapa alipo,” alisema. “Sasa hivi Young Killer anakaribia kumaliza nyumba yake, familia inamtegemea kwa sababu mimi niliona akifanya huu muziki na umri mdogo unaweza ukamwathiri, lakini nikashanga kaamua kuondoka nyumbani na kwenda Dar. Young Killer aliondoka tu bila kuniaga, siku hiyo akanipigia simu akaniambia ‘mama save hiyo namba yangu, mimi nipo Dar’.
Nikamuuliza kuna nini huko akasema ‘mama hebu niache kwanza’. Baada ya hapo nilikuwa nawasiliana na kaka yake ananiambia ‘mdogo wangu yupo hapa nyumbani’ nikamwambia ‘shule vipi? wewe utakaaje na mwenzako wakati unajua ni mwanafunzi!’ Akaniambia ‘mama nikiishi naye vizuri wewe naomba uniache kwa sababu naona hii ni talent yake hatoweza kusoma tena sasa hivi’ nikasema ‘mrudishe’ akasema ‘mama muache kwanza tusimrudishe,” aliongeza Mama Msodoki. 

“Huyu mtoto nilimpiga mpaka nikahisi kuna tatizo litamkuta, yaani nilimpiga mapaka akazimia, mpaka majirani wanasema ‘muache’ lakini unaona nikimuacha wakati nimetoa ada ili asome shule wanakwambia ‘achana naye’. Mimi sikupenda nimuache, kwasababu katika familia yangu ya marehemu Mzee Msodoki wote ndugu zake wamesoma sasa nilikuwa siwezi kumuacha asiende shule. Mimi sikutaka asifanye muziki nilikuwa nataka asome kwanza.” 
Katika hatua nyingine Mama Msodoki alielezea tabia ya mwanae wakati akiwa mdogo mpaka alivyoingia kwenye muziki. 

“Hakuna mtoto aliyekuwa mtiifu kama huyu,” anasema. “Alikuwa Akitoka shuleni anafika nyumbani muda unaotakiwa, huwezi ukamkuta ametoka nyumbani katika muda ambao hakutakiwa kutoka. Hayo mazoezi yake ya muziki alikuwa anafanya labla muda wa shule, kwasababu muda wa kutoka shule ukifika anakuwa yupo nyumbani. Nikitoka kazini ninamkuta yupo nyumbani na anajisomea huwezi amini. Kwahiyo hata mtu anapokwambia kwamba ‘mwanao anafanya hivi’ huwezi ukamwamini. Lakini mpaka nikafikia hatua nikafuatilia shule mahudhurio yake kwakweli yakawa sio mazuri.”
Source:Bongo5.com

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger