JE, KUNA AFADHALI UKIMFUMANIA MUMEO NA DEMU MZURI KULIKO WEWE? SOMA UJUE ZAIDI

WIVU ni neno lililosheheni maana nyingi kwenye maisha ya kila siku. Mtu anaweza kukasirishwa na mafanikio ya mwingine, huo pia ni wivu.Lakini ile tabia ya mwenza kutoka kimapenzi na mwingine, wengine wanaita usaliti ni wivu mkubwa zaidi na unagharimu maisha ya wengi duniani.
Zipo kumbukumbu zinazoonesha kwamba, mamilioni ya watu wamepoteza maisha kutokana na kukutwa au lugha rahisi kufumaniwa na wenye wenza wao.
Kuna wenza wanaofumania na kuchukua hatua ya kuua au kumtia kilema mgoni wake kutokana na wivu na hasira, hasa wanaume. Lakini pia wapo wanaofumania na kujishusha wakijua hatua zaidi inaweza kumweka pabaya, hawa ni wale wanaopambana na hasira na wivu. Lakini hapo ndipo hutokea talaka au mapenzi kuchuja kama si kunyauka kabisa.
DHANA INAYOCHANGANYA WENGI
Leo kwenye mada yangu hii sipendi kuingia kwa undani kwenye wivu unavyogharimu maisha ya watu bali nataka kugusia dhana iliyojengeka kwa baadhi ya watu wakirahisisha hasira na haiba kwa mtu wanayemfumania.

Si ajabu kusikia mitaani wanawake wakisema ‘mimi nikimfumania mume wangu nitamwangalia huyo mwanamke niliyemfumania naye. Kama wa hovyohovyo nitamshangaa sana mume wangu.’ Au wengine husema, ‘afadhali nimfumanie mume wangu na demu mzuri ambaye hata mimi nitasema alikuwa na haki, lakini siyo unamfumania na mwanamke yuko kama kinyago’.
SIMULIZI YA AJABU
Siku za karibuni, kuna mwanamke mmoja niliwahi kuzungumza naye ambapo alikiri kuwa, mumewe aliwahi kutembea na msichana asiyemjua jina wala makazi yake.Alisema alikuwa akimwambia mumewe kwamba kama huyo msichana ni mzuri kuliko yeye sawa, lakini kama ana sura ‘ngumu’ (mbaya) atamshangaa sana.

“Ingawa mume wangu alikataa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamke mwingine, lakini mimi nilihakikishiwa na mashoga zangu ambao walishamuona mara kadhaa wakitanua kwenye mabaa.
“Niliwauliza mashoga zangu huyo msichana anafananaje lakini hawakunipa jibu moja, mwingine alisema mrembo mzuri, mimi simwingii, ana sifa zote,  mwingine akasema hamna kitu wanja wenyewe anapaka ule wa ‘sina bwana’ (kunyoa nyusi na kupaka wanja kwa juu).

“Siku moja nilibahatika kumfumania mume wangu baada ya kuambiwa ameingia gesti na huyo msichana. Wakati nakwenda kufumania kiu yangu kubwa ilikuwa kutaka kumwona huyo msichana yupoje? Kama mimi au amenizidi.
“Nilipenda awe amenizidi maana kama nitakuwa nimemzidi  nitamshangaa sana mume wangu. Kufika kweli alikuwa msichana mzuri sana, simwingii kwa hata chembe. Kidogo hiyo ilinishusha hasira na wivu,” anasimulia Mwanaidi  Mkwazu, mkazi wa Sinza, Dar.
Itaendelea toleo lijalo.

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger