Sherehe hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Posta jijini Dar ambapo mbali na watu wa kawaida, wake wa viongozi mbalimbali nchini pamoja na baadhi ya wasanii wa Bongo Movies walihudhuria.
Miongoni
mwa matukio ambayo yaliibua mshangao kwa waalikwa ni bibi harusi
mtarajiwa (Lucy) kutinga ukumbini hapo akiwa ndani ya baiskeli yenye
magurudumu matatu (guta) akiwa na wapambe wake ambao walikuwa peku
miguuni.
Kwenye guta hilo lililotengenezewa kibanda cha asili kilichowekwa
nyasi juu, Lucy alikaa ndani yake huku wapambe wake wakiwa wameshika
nyungo ndogo kuashiria asili ya Mtanzania.Kama hiyo haitoshi, Lucy aliwaacha hoi waalikwa kutokana na vazi lake ambalo ni tofauti na wanavyovaa wengine katika sherehe kama hiyo kwani alitinga kipensi kifupi kwa ndani chenye rangi ya bendera ya Tanzania huku kwa nje kikifunikwa na kitambaa chepesi.
“Ama kweli hii ni ya aina yake, hebu angalia nguo yake alivyoitengeneza kwa kweli inavutia sana, full utamaduni,” alisikika mmoja wa watu walioudhuria sherehe hiyo.
Ulipofika wakati wa kufungua shampeni, nayo ilikuwa ya aina yake. Aliandaliwa pombe ya kienyeji ya mkoani Ruvuma ijulikanayo kama Kangara ambayo aliiweka ndani ya kibuyu kidogo huku akipita kugongesha na wageni waalikwa.
Baadhi ya marafiki zake waliotoka nchi mbalimbali akiwemo muigizaji kutoka nchini Italia, Angela Howell, alidondosha chozi la furaha alipoona waalikwa wanakula ndafu badala ya keki kama ilivyozoeleka na wengi.
Lucy Komba anatarajia kufunga ndoa hivi karibuni na mchumba wake aitwaye Stanley, raia wa Denmark. Watafanya sherehe kubwa Bongo na baadaye kuangusha nyingine Denmark.
No comments:
Post a Comment