Msanii wa muda mrefu katika filamu Bongo, Salome Urassa maarufu kama
Thea, amejinasibu kuwa kutovaa kwake pete ya ndoa haimaanishi chochote
kwa vile kitu hicho siyo muhimu.
Akizungumza na paparazi wetu juzikati, Thea alisema awali alikuwa
akivaa pete, lakini bahati mbaya ilipotea na kupotea huko hakumaanishi
kwamba ndoa yake imepotea.
“Sitaki kuamini kabisa kama ndoa ni pete, ninachojua ni kwamba siku
zote ipo moyoni, unaweza kuvaa hata pete kumi kidoleni, lakini kama
haina amani ni kazi bure tu, mimi sina lakini kama nina furaha kwenye
ndoa yangu hakuna neno,” alisema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment