STAA wa filamu Bongo ambaye amejikita kumtumikia
Bwana kwenye wokovu, Ruth Suka ‘Mainda’ amesema kamwe hawezi kuainisha
sifa za mwanaume anayehitaji aolewe naye kama ilivyo kwa mastaa wengine
kwa kuwa jukumu hilo ni la Mungu.
Akipiga stori na paparazi wetu, Mainda alisema japo umri wake
unaruhusu kuolewa hawezi kuweka wazi sifa za mwanaume anayehitaji awe
wake kwa kuwa huenda sifa anazozihitaji Mungu hajampangia kuolewa na mtu
wa aina hiyo.
“Kwenye maono naona kabisa mume wangu yupo karibu ambaye Mungu
ameniandikia, sasa siwezi kusema nahitaji mwanaume mwenye sifa zipi
sababu nikisema nahitaji awe hivi kumbe Mungu hajanipangia huyo,”
alisema Mainda.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment