ANA hoja? Siku chache baada ya gazeti pacha la hili,
Ijumaa Wikienda, toleo la Jumatatu iliyopita kuripoti juu ya utajiri
mkubwa wa staa wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja ‘K’, mumewe Faraji
Agustino amempigia saluti na kumuomba amtoe gerezani.
KWANI ILIKUWAJE?
Machi mwaka jana, Faraji
alihukumiwa kifungo cha miaka saba jela au faini ya zaidi ya Sh. milioni
200 baada ya kupatikana na hatia ya kutakatisha fedha haramu kwenye
Benki ya NBC, Tawi la Dar ambapo jamaa huyo alishindwa kulipa kiasi
hicho cha fedha na kujikuta ‘akiozea’ Segerea au Segedansi kama
wanavyoita mastaa wa Kibongo.
UTAJIRI WA GHAFLA
Katika msala huo, Kajala
alihukumiwa miaka mitano jela au faini ya Sh. milioni 13 kwa kukutwa na
hatia ya kuuza nyumba yao iliyowekwa kizuizini na Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa (Takukuru) ambapo alilipiwa shilingi Milioni 13 na
Wema Isaac Sepetu na sasa anapeta mtaani na utajiri wa ghafla.
HOJA YA MSINGI
Baada ya kuokolewa jela na Wema,
Kajala ametembelewa na utajiri ambapo amekuwa akitanua mitaa mbalimbali
ya Jiji la Dar, akisukuma magari ya kifahari, kupanga ghorofa maeneo ya
Sinza-Madukani anayolipia Sh. milioni 3.2 kwa mwezi, akimiliki kampuni
ya kuzalisha sinema ya Kay Entertainment huku akaunti yake ikiwa imenona
kwa mamilioni kadhaa.
GEREZANI SEGEREA
Hivi karibuni, ‘mtu wetu’
alikwenda kumtembelea Faraji kwenye Gereza la Segerea, Dar ambapo
alipata nafasi ya kutoa la moyoni juu ya mkewe Kajala ambaye alifunga
naye ndoa kanisani miezi michache kabla ya kukutwa na msala huo.
Akizungumza kwa huruma, Faraji alisema habari za Kajala kuwa na
utajiri wa kutupwa alianza kuzisikia kwa ndugu zake hivyo kumuomba staa
huyo kumkumbuka kwenye ufalme wake.
Jamaa huyo alisema kila akikaa huwa anakumbuka good time (kipindi cha
matanuzi) yao ambapo ilikuwa ni bata mwanzo mwisho hasa nyakati za
wikiendi.
Kwa mujibu wa mtu wetu huyo, Faraji alimwambia: “Mwambieni K akumbuke
yeye ni mke wangu. Nimemsaidia kwa mengi, asiniache nateseka huku yeye
anachezea pesa ambazo anaweza kunilipia na nikatoka kifungoni. Pia
akumbuke ahadi yetu ya ndoa kanisani na jinsi tulivyoishi kwa upendo.
“Bado ni mke wangu, bado nampenda sana. Nilisikia alishavua pete ya
ndoa lakini ukweli ni kwamba bado mapenzi yetu yapo palepale. Kama kweli
Kajala amepata utajiri naomba anitoe gerezani, sitamsahau maisha yangu
yote. Kama nilivyoahidi kanisani, nitampenda na kumtunza hadi kifo
kitutenganishe.”
Chanzo hicho kilidai kwamba Faraji alisema Kajala amuonee huruma,
azungumze na wadau wake wote wamtoe gerezani halafu atajua jinsi ya
kurejesha fedha hizo.Habari nyingine kuhusu suala hilo ilisemekana
kwamba jamaa huyo ametengeneza netiweki akiwa gerezani kupitia kwa watu
wake wanaomtembelea ambao wapo tayari kuungana na staa huyo ili
kufanikisha jambo hilo.
INAWEZEKANA?
Akizungumza na gazeti hili, mmoja
wa wanasheria wenye uzoefu na kesi za mastaa aliyeomba hifadhi ya jina
alisema kwamba jambo hilo linawezekana endapo mteja (mume wa Kajala)
ataomba kesi yake ifanyiwe ‘reference’ (mapitio).
“Unajua haya ni mambo ya kisheria, kwa mtu wa kawaida anaweza
asiyaelewe kirahisi lakini uwezekano upo bila hata kukata rufaa.“Faraji
alihukumiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu (Dar). Kitakachofanyika
ni kwamba kama akitaka kesi yake itafanyiwa reference kwenye mahakama ya
juu.
“Baada ya hapo Faraji au wakili wake anaweza kuomba kulipa
faini badala ya kifungo kwa sababu hukumu ilisema kifungo cha miaka saba
au faini ya hiyo shilingi milioni 200.
“Kama kweli Kajala ana hiyo fedha si mbaya akafanya hizo process (taratibu), akamtoa mumewe,” alisema ‘loya’ huyo.
KAJALA ANASEMAJE?
Baada ya kujazwa data hizo,
Jumatano iliyopita Ijumaa lilimtafuta Kajala ambaye simu yake haikuwa
hewani kila ilipopigwa na hata alipofuatwa nyumbani kwake hakuwepo
lakini kwenye makabrasha kulikuwa na maelezo yake juu ya mumewe
alipohojiwa siku kadhaa zilizopita.
Kwa mujibu wa Kajala, Faraja bado ni mumewe na huwa anakwenda
gerezani kumuona kila wikiendi na anatamani awe huru ili waendelee na
maisha kwani hawakuwa wamefaidi penzi lao, hata mtoto walikuwa
hawajapata.
MARAFIKI WANASEMAJE?
Marafiki wa wanandoa hao
waliozungumza na Ijumaa walisema kwamba kama kweli Kajala ana nia hiyo,
basi afanye hiv yo kwani itakuwa thawabu kubwa kwake kama alivyofanyiwa
na Wema aliyemnusuru kifungo cha miaka mitano jela.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment