Baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo waliliambia Ijumaa Wikienda kwamba kuna kafara ilitolewa na mmoja wa watu waliohusika katika ajali hiyo.“Haiwezekani magari yakagongana uso kwa uso sehemu nyeupe kama ile, hata kama ni uzembe, ajali hii ni zaidi ya uzembe,” alisema kijana mmoja aliyeshuhudia ajali hiyo aliyeomba hifadhi ya jina lake kwa imani hiyo ya kishirikina.
Aliongeza kwamba kuna wafanyabiashara wengi walikuwa kwenye mabasi hayo na baadhi yao wanapenda mambo ya kishirikina.
Baadhi ya miili ya watu waliofariki katika ajali hiyo.
Hata hivyo, alipobanwa zaidi, hakuwa tayari kutoa ufafanuzi.Shuhuda mwingine aliyejitambulisha kwa jina moja la Maduhu alidai kuwa chanzo cha ajali hiyo ni basi la J4 ambalo lilikuwa likijaribu kulipita gari dogo aina ya Nissan Terano lenye nambari za usajili T 332 AKK katika sehemu ambayo mbele kulikuwa na daraja linaloweza kupitisha gari moja kwa wakati mmoja.
Guldoza
likifanya kazi ya kuichomoa gari ndogo aina ya Nissan Terano lenye
namba ya usajili T 332 AKK lililosukumwa na basi kwenye ajali hiyo mpaka
kuingia mtoni. Gari hili ilikuwa na watu watatu, ambapo wawili
wamefariki dunia na mmoja kujeruhiwa.
“Ukweli wapo watu wanadai kuwa hii ni kafara ili majini wanywe damu
na mambo yao yaende vizuri lakini ukweli ni kwamba basi hilo lilikuwa
kwenye mwendo kasi, lililisukuma ubavuni gari dogo ambalo halikuweza
kuhimili na kutoka kwenye njia na kwenda kuingia mtoni nalo kugongana na
basi la Mwanza,” alisema Maduhu.Jumamosi iliyopita, gazeti hili lilipokea ripoti kuwa bado haijafahamika ndani ya mabasi hayo kulikuwa na abiria wangapi ambapo ilidaiwa kuwa waliokufa na majeruhi walikuwa wameongezeka.
No comments:
Post a Comment