WEMA AANGUA KILIO CHA MBWA MWIZI

Beautiful Onyinye, Wema Abraham Sepetu ametoa kioja cha aina yake kwa kuangua kilio baada ya kuambiwa kuwa mbwa wake aliyepotea amepatikana na alipokwenda kumfuata akaambulia patupu.
Mbwa wa staa wa filamu Bongo, Wema Abraham Sepetu aliyepotea.
Tukio hilo lililowaacha watu midomo wazi lilitokea juzikati maeneo ya kishua, Masaki jijini Dar, ambapo staa huyo alionekana kukatishwa tamaa kwani alipokuwa anatoka nyumbani aliamini kabisa anakwenda kukabidhiwa mbwa wake aitwaye Vani aliyepotea miezi michache iliyopita.
“Nilipoambiwa amepatikana kwanza nilijenga picha kwamba hatimaye furaha yangu imerejea, nilianza kuvuta picha ya kipindi cha nyuma alipokuwepo nyumbani lakini nilipokwenda nikakuta ndivyo sivyo,” alisema Wema na kuongeza:
Wema Abraham Sepetu akiwa na mbwa wake, Vanny kabla ya kumpoteza.
“Uwiiii jamani Vani wangu ndio sitomuona tena naumia sana kuondokewa na Vani nitamkumbuka daima, sijui amekufa au vipi!” alisikika Wema kiasi cha watu waliokuwepo eneo hilo kumshangaa wakijiuliza ni mbwa tu aliyemsababisha alie kilio mithili ya kuomboleza.
Wema ametangaza dau la shilingi milioni moja kwa mtu yeyote atakayefanikisha kupatikana kwa mbwa wake huyo ambaye mwenyewe anasema alikuwa faraja kubwa kwake pindi anapokuwa nyumbani.

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger