CHUCHU AWAJIA JUU WANAOIPONDA ‘KAPO’ YAO

MALOVEE! Staa wa filamu Bongo, Chuchu Hans, amewashukia watu wanaoiponda ‘kapo’ yake na mwigizaji Vincent Kigosi ‘Ray’ na kusema hata iweje, mambo yao yatakwenda kama walivyopanga.
Staa wa filamu Bongo, Chuchu Hans.
Chuchu alisema katika maisha ya mwanadamu kama Mungu amepanga kitu siku zote kitatimia hivyo anaamini wanaopinga uhusiano wao kwa maneno ya chinichini na kwenye mitandao ya kijamii ni maadui lakini hawatashinda.
“Najua kabisa nina maadui wengi sana lakini naamini Mungu atasimama wanaiponda sana ‘kapo’ yetu lakini Mungu akipanga kitu siku zote lazima kitatimia  hakuna ubishi,” alisema Chuchu.
Staa wa filamu Bongo, Chuchu Hans akiwa na mpenzi wa Vincent Kigosi ‘Ray’.
Kabla ya kuwa na uhusiano na Ray, Chuchu aliwahi kuolewa na mtangazaji Frank Mtao ambaye inasemekana wameshamwagana.

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger