NGOMA nzito! Kauli ya sexy lady wa sinema za
Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ kuwa yupo tayari
kumtumikia msanii mwenzake Kajala Masanja ‘K’ kwenye kampuni yake ya KAY
Entertiment tena bila malipo yoyote, imetafisiriwa kuwa ni kejeli.
Hivi karibuni Wema alikaririwa akisema: “Nakubali kwamba Kajala
anaweza kuwa na maisha mazuri ya kiasi hicho na akanifanya mfanyakazi
wake katika kamusi yake kwa sababu sioni cha kumfanya ashindwe kuwa
hivyo, naamini anaweza kuniajiri na wala sina kipingamizi! hahahaa!”
Baada ya kauli hiyo ya Wema, mashabiki wake waliikataa kwa maelezo
kuwa alilenga kumkejeli Kajala ambaye awali aliwahi kumwajiri kwenye
kampuni yake ya Endless Fame Production.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment