Msiba! Bado bundi wa vifo anaendelea kung’ang’ania
tasnia ya sinema za Kibongo kufuatia kifo cha ghafla cha msanii wa Bongo
Muvi, Mariam Juma ‘MC Chimamy’ ambaye amefariki dunia ghafla baada ya
kupatwa na kifafa cha mimba, ugonjwa uliomkuta muda mfupi kabla ya
kujifungua.
Mauti hayo yalimkuta MC Chimamy wikiendi iliyopita baada ya
kukimbizwa kwenye Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar, akiwa tayari na
hali mbaya kwani kabla ya hapo alianzia Hospitali ya Palestina, Sinza
ambapo alilazimika kukimbizwa katika hospitali hiyo ya Wilaya ya
Kinondoni ili kunusuru maisha yake na kiumbe alichokuwa nacho tumboni.
Msiba huo umezua simanzi kubwa kwa wasanii wenzake hasa Vanita Omary,
Halima Yahya ‘Davina’, Yvonne-Chery Ngatwika ‘Monalisa’, Mariam Kakwaya
na wengine kwani alikuwa ni mtu wao wa karibu na siku aliyokutwa na
umauti alikuwa amepangwa kuwa mshereheshaji wa shughuli ya Davina ya
kibao kata iliyofanyika Bamaga-Mwenge, Dar.
“Msiba huu umenishtua sana, sikutarajia kama Chimamy angetutoka
kimchezo hivi, ukweli nimeumia sana na sina la kusema, namshukuru Mungu
kwa kazi yake,” alisema Vanitha.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment