BAADA YA KUWA NA BIFU LA MUDA MREFU NA DIAMOND SASA BABY MADAHA ASALIMU AMRI NA KUAMUA KUACHA MUZIKI PAMOJA NA FILAMU, SOMA HAPA KUJUA ZAIDI

IKIWA imepita miezi kadhaa tangu anaswe katika mtego  wa kujiuza,  staa wa Bongo, Baby Madaha ametangaza kuachana na sanaa ya muziki na filamu kwa maelezo kuwa amechoshwa na  maisha ya presha. Akiongea  na  mwandishi wetu  juzikati jijini Dar es Salaam, Madaha alisema ishu ile imemsababishia matatizo makubwa ya kifamilia na hata kibiashara, hivyo kujutia mchezo mzima ulivyokuwa.

Alisema filamu anayoisambaza (usisahau kulike page yetu ya mdadisi mambo ka kuclick hapa) kwa sasa na kibao chake cha mwisho kukitoa cha Mr. Dj ndizo zitakazofunga pazia la mambo ya sanaa kwa upande wake.

 “Nimeamua kuachana na sanaa kabisa, siwezi kuishi maisha ya presha yasiyo na uhuru. Nitarudi kwenye fani yangu niliyosomea (hakutaka kutaja), maana naishi maisha ambayo hayana amani kabisa,” alisema.

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger