skip to main |
skip to sidebar
SNURA ARUDIWA NA MAJANGA YAKE, YASOME HAPA UYAJUE MAJANGA YALIYOMPATA
BAADA ya hivi karibuni kufungiwa video ya wimbo wake, staa wa muziki
na filamu Bongo, Snura Mushi amesema ameendelea kuandamwa na majanga
ambapo hivi karibuni alipata msiba wa babu yake huku mdogo wake akipata
ajali.
Akizungumza
kwa huzuni, Snura alisema mwaka huu umekuwa wa majanga kwake kwani babu
yake huyo alimlea na kushika nafasi ya baba yake tangu alipozaliwa hadi
kufikia utu uzima.
“Ukweli nimeumia sana na mwaka huu umekuwa ni wa majanga kwangu kwani
babu yangu huyo nilikuwa namuita baba kwa sababu yeye ndiye aliyenilea
mpaka nikafikia umri huu nilionao, mdogo wangu naye alipata ajali mbaya
yuko hoi hospitali, utumbo ulitoka nje na kwenda kufanyiwa oparesheni,
nimechanganyikiwa,” alisema Snura.
No comments:
Post a Comment