Showing posts with label SNURA. Show all posts
Showing posts with label SNURA. Show all posts

WAJUA SNURA ANAKITU GANI TUMBONI? BASI MSIKILIZE HAPA AKIFUNGUKA

snuraBaada ya kusikika maneno mengi sana juu ya uhusiano wa Snura na mpenzi wake anayefahamika kwa jina la Dj Hunter,Soudy Brown amekuja na taarifa ambayo inahusu hali ya Snura kwa sasa ambapo inasemekana ni Mjamzito.
Read more >>

SNURA AFUNGUKA KUHUSU RUSHWA YA NGONO

Msanii  wa  muziki  na  filamu  Snura  Mushi  amebainisha  kuwa  rushwa  ya  ngono  kwa  wanawake  ni  kikwazo  kikubwa  kinachowakwamisha  wanawake  kutimiza  ndoto  zao...

Snura  aliamua  kungukia  suala  hilo  ili  kuwatetea  wanawake  wanaoombwa  rushwa  ya  ngono  ili  kupewa  kazi, kwa  kusema  ni  kitendo  cha  kinyama  kwani  wengi  wanakuwa  ombaomba  kwa  sababu  tayari  wamekosa  kazi  kutokana  na  kulazimishwa  kitendo  hicho.....

"Wanawake  wanaweza  lakini  wengi  wanakatishwa  tamaa  na  baadhi  ya  watu  wanaotumia  nafasi  zao  vibaya. Unakuta  mwanamke  kafanya  vizuri  na  ana  uwezo  mkubwa  lakini  suala  la  rushwa  ya  ngono  ndo  linalowavunja  nguvu  na  kujikuta  wakiwa  tegemezi  katika  maisha  yao," alisema Snura.
Read more >>

SNURA ANA MIMBA, BABA KIJACHO HUYU HAPA


Snura Mushi

KWA mujibu wa mtu wa karibu wa mwanadada Snura ambaye jina lake tumelisunda kapuni ameinong'oneza Website hii kwamba Snura alionyesha dalili zooote za ujauzito wakati wakiwa safarini kutoka Iringa kuja Dar baada ya kutoka katika tour ya Kilimanjaro, Dalili hizo moja wapo ikiwa kutapika mara kwa
mara.. Aliendelea kufunguka kuwa ujauzito huwo asilimia kubwa utakuwa wa DVJ Hunter wa Maisha Club ya Jijini Mbeya. Mmh.. mi napita tu!


Read more >>

SNURA: MIMI NA DJ TUNAPENDANA SANA HIVYO MTASUBIRI SANA TUACHENI, SOMA MANENO YA SNURA HAPA

MAMAA Majanga, Snura Mushi amekiri kutoka katika uvungu wa moyo wake kuwa amedhibitiwa vilivyo na penzi la jamaa anayetoka naye kwa sasa aitwaye DJ Hunter hivyo hawezi kuachika.

Mamaa Majanga, Snura Mushi akijiachia kijanja na mpenzi wake DJ Hunter.
Akipiga stori na mwandishi wetu, Snura alifunguka kwamba tofauti na wanaume wote aliowahi kuwa nao, DJ Hunter wanapendana kwa dhati na anaamini ndiyo chaguo sahihi kwake.  “Sijawahi kuwa na mpenzi nikamtambulisha kwenye media bila kuwa nimempenda kwa dhati, tunapendana sana na Hunter, hatuwezi kuachana kwa mipango ya binadamu,” alisema Snura
Read more >>

SNURA MUSHI AJITOSA KATIKA BIFU LA WEMA, KAJALA

MSANII wa filamu na muziki, Snura Mushi ameingilia kati ugomvi wa wasanii wenzake, Wema Sepetu na Kajala Masanja na kuwaagiza wamalize tofauti zao.
Msanii wa filamu na muziki, Snura Mushi a.k.a mama majanga.
Wasanii hao ambao wameingia kwenye bifu la kufa mtu kufikia hatua ya kuanikana kwenye vyombo vya habari huku chanzo kikubwa kikitajwa ni shilingi milioni 13 ambazo Wema alimlipia Kajala kama faini ya kesi ya kuuza nyumba iliyokuwa imewekwa rehani kisheria iliyokuwa ikimkabili mahakamani.
Nyumba hiyo iliwekwa rehani kutokana na mume wa Kajala, Faraja Agustino kushitakiwa kwa kosa la kutakatisha fedha haramu.
Wema na Kajala.
Snura amewataka Wema na Kajala kutoangalia nani ana makosa, wamalize tofauti zao.
“Nawashauri wenzangu wasigombane na kuwekeana vinyongo hiyo ni kama wanawapa watu faida,

nawaomba wamalize kwani haipendezi kabisa kwa jinsi walivyokuwa wameshibana. Kama mmoja anaona amemkosea mwenzake ajishushe na kuomba msamaha,” alisema Snura.
Read more >>

HUYU NDIOMPENZI WAKE SNURA

Snura Mushi na Dvj Hunter wa Club Maisha Ya Mjini Mbea wakiwa katika Poz la maha..!

Kwa mujibu wa mtu wa karibu aliozinasa picha hizo zilizopigwa huko mkoni Mbeya alisisitiza kwamba jina lake lisitajwe humu mtandaoni, Pia alizidi kufunguka kwamba kabla hajakwanyua picha hizo alibahatika kusikia maneno ya Snura kama ifuatavyo: Mimi kwa huyu jamaa sina ujanja na kamwe sitosikia la mtu ng'o! Mmmh.. Penda sana Hunter...!
Jamaa aliishia hapo akasema alikuwa anapita tu!
Du! Hatari tupuuuu...! Yani ni shidaaaaa...!
DVJ Huntuer katika pozzzz!
DVJ Hunter katika moja na mbili..!
 
Read more >>

SNURA ARUDIWA NA MAJANGA YAKE, YASOME HAPA UYAJUE MAJANGA YALIYOMPATA

BAADA ya hivi karibuni kufungiwa video ya wimbo wake, staa wa muziki na filamu Bongo, Snura Mushi amesema ameendelea kuandamwa na majanga ambapo hivi karibuni alipata msiba wa babu yake huku mdogo wake akipata ajali.
Akizungumza kwa huzuni, Snura alisema mwaka huu umekuwa wa majanga kwake kwani babu yake huyo alimlea na kushika nafasi ya baba yake tangu alipozaliwa hadi kufikia utu uzima.
“Ukweli nimeumia sana na mwaka huu umekuwa ni wa majanga kwangu kwani babu yangu huyo nilikuwa namuita baba kwa sababu yeye ndiye aliyenilea mpaka nikafikia umri huu nilionao, mdogo wangu naye alipata ajali mbaya yuko hoi hospitali, utumbo ulitoka nje na kwenda kufanyiwa oparesheni, nimechanganyikiwa,” alisema Snura.
Read more >>

SNURA ASEMA ETI WABAYA WAKE WANATAKA KUHAKIKISHA ANASHUKA KIMAENDELEO, SOMA HAPA KUJUA ZAIDI

STAA aliyeliteka soko la mduara kwa kibao chake cha Majanga, Snura Mushi amesema watu wenye chuki na yeye wamepanga njama za kumshusha kwenye chati kutokana na maendeleo yake.
Snura Mushi.
Akipiga stori na paparazi wetu juzi, Snura alisema: “Nashangaa sana ninapofanya jambo zuri halafu watu wanaligeuza kuwa baya ili nichafuke jina na kunipunguzia mvuto kwa mashabiki wangu.”
Chanzo cha yote ni baada ya mwanadada huyo kupiga shoo kwenye Ukumbi wa Buliyaga, Temeke, Dar siku chache zilizopita, kundi la watu wasiojulikana walianza kueneza taarifa kuwa alifanya vibaya na mashabiki wakamtaka ashuke jukwaani jambo ambalo alisema halikuwa na ukweli wowote.
Read more >>
 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger