WAANDAAJI
wa shindano la Tuzo za Filamu Tanzania lililopewa jina la Action &
Cut Viewers Choice Award 2013 wamezitaja filamu zitakazopigiwa kura na
watazamaji kupitia kipindi cha Action & Cut kinachorushwa na runinga
ya Channel Ten pamoja na vipengele husika.Mratibu wa shindano hilo, Bond Bin Sinnan alitaja vipengele vinavyoshindaniwa, wasanii na filamu zao kwenye mabano kuwa ni mwigizaji bora; Jacob Stephen (Shikamoo Mzee), Mohammed Mwikongi (Waiting Soul), Simon Mwampagata ‘Rado’ (Mahaba Niuwe), Hemed Suleiman ‘PHD’ (Stella), Steve Mengere ‘Steve Nyerere’ (Get Out), na Salim Mohammed (Bado Natafuta).
Mwigizaji bora wa kike; Rose Ndauka (Waiting Soul), Irene Paul (Love & Power), Wastara Juma (Mr & Mrs Sajuki), Irene Uwoya (Questions Mark), Elizabeth Michael ‘Lulu’ (Foolish Age), na Jackline Wolper (Mahaba Niuwe).
Bond, alitaja walioingia kipengele cha waigizaji bora wanaochipukia upande wa wanaume ni Rammy Valid (Fan’s Death), Mohammed Mussa (Mbegu), Gerry wa Rhymes (Stella), huku wa kike ni Wellu Sengu (Matilda), Janeth Lameck (Bikira Kidawa), na Najma Dattan (Fan’s Death).
Kwa upande wa waongozaji bora ni Vincent Kigosi ‘Ray’ (Twisted), Issa Mussa ‘Cloud’ (Shahada), John Lister (Pumba), Jackson Kabirigi (Nguvu ya Imani), Lamata (Mr & Mrs Sajuki), na Kulwa Kikumba ‘Dude’ (Melvin).
Filamu bora zinazoshindaniwa na kampuni zilizotengeneza kwenye mabano ni ‘Twisted’ (RJ Film Company), ‘Shikamoo Mzee’ (Jerusalem Film Company), ‘Tikisa’ (Nisha’s Film Company), na ‘Mr & Mrs Sajuki’ (Wajey Film Company).

No comments:
Post a Comment